Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia Julai 2020 umeongezeka hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.2

Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia Julai 2020 umeongezeka hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.2

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Jedwali Namba 1 hapo juu linaonesha kuwa, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwamwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.74 mwezi Juni 2020 kutoka 117.03 mwezi Juni 2019. Mfumuko wa Bei kwa Bidhaa za Vyakula na Bidhaa zisizo za Vyakula Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Juni 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 mwezi Mei, 2020.

Mfumuko wa Bei kwa kipimo cha mwaka kwabidhaa za vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawanikwa mwezi Juni, 2020 umepungua hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande mwingine, badiliko la Fahirisi za Bei kwa bidhaa zisizo za vyakula kwa mwezi Juni 2020 limeongezeka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.4 mwezi Mei, 2020.
 

Attachments

Back
Top Bottom