Deeboyfrexh
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 3,417
- 5,579
Uchumi unafunguka na watu wanalia njaa humu!We kaa hapo kijiweni uendelee kuisubilia utaona moto wa maisha.
Saizi uchumi unafunguka , uwekezaji unaongezeka changamkia fursa.
Subilia kulaumu serikali utaisoma namba
Una maanisha wale madogo polepole, kheri James, Kihongosi, masanja mkandamizaji na paul makonda etiii.Wale washangiliaji wako wapi
Machadema na waliokaa vijiweni wanasubilia kulaumu kwa nini wasilie njaa?..Uchumi unafunguka na watu wanalia njaa humu!
Kawaida tu ipande ishuke tutaishiTzn sio Dar kwa hiyo pambaneni na hali yenu..
Uchumi wa nchi kama hii ndio jamaa anasema it will never happen. Marekani ilitokea GED miaka ya 1920s na mdororo wa uchumi mwaka 2008 wakati inaongoza uchumi wa dunia. Ujerumani iliwahi fikia inflation ya 29,500% (sijakosea kuandika) yani walikuwa wanakaa siku tatu na masaa kadhaa bei zinakuwa twice. Jumatatu saa 1 ukinunua kilo kwa 200, Alhamisi jioni hiyo kilo inauzwa 400. Kwa siku walikuwa na inflation ya over 20%Kusema it will never happen hapo ndio ujinga wako ulipojidhihirisha bila kificho.
Kwenye uchumi anything can happen. Kusema it will never happen inaonyesha kabisa jinsi ulivyo mweupe kichwani.
Na ndio maisha siku zote,Mfuko wa simenti ulikuwa 4500 2010 leo 20,000 ..Kawaida tu ipande ishuke tutaishi
Kuna watu wananunua nyama kg 1 ,zaidi ya hiyo
I pande ishukke ipande tutaishi
Ova
Mkoani ChatoMtambani ndio wapi?
Nyie ndio mlituharibia nchi,huko ipande kabisa mkome🏃🏃Mkoani Chato
Fresh tuNa ndio maisha siku zote,Mfuko wa simenti ulikuwa 4500 2010 leo 20,000 ..
Nchi iko Uchumi wa Kati gharama za maisha kupanda ni kawaida.
Tozo zote ziliwekwa kwa sheria ya Bunge na Kati ya hizo ziko ambazo zinaweza kuwa adjustable lakini huwezi futa lazima zirudi Bungeni na zingine huwezi hata kuzibadilisha ndio maana Ili kuzifuta lazima warudishe mswaada wa sheria Bungeni.Ameadjust lini tupe walaka wa EWURA aseee???
Nilichosikia wanakwenda kurekebisha sheria ya kupunguza tozo. Yaan baada ya mvua ya tozo kuwa nzito tena ya mawe na upepo walau watatupa mwamvuli kupunguza makali lakini kuloana kupo pale pale.
Una maanisha wale madogo polepole, kheri James, Kihongosi, masanja mkandamizaji na paul makonda etiii.
Tusimsahau kibajaji na kasheku msukuma
Tutasikia mengi kwa hali tunayoenda nayo.Bidhaa za nyama, gesi ya kupikia, mkaa na viazi mviringo zimetajwa kuongeza mfumuko wa bei kutoka asilimia 3.8 Agosti hadi asilimia 4.0 kwa Septemba mwaka huu.
Taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Oktoba 8 jijini Dodoma, imetaja bidhaa nyingine zilizoongeza mfumuko wa bei ni ngano na maziwa ya unga.
Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja alisema sababu za kuongeza mfumuko ni kutokana na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma.
Minja alisema mabadiliko hayo ni kwa mwaka ulioishia Septemba ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Agosti 2021.
Amesema badiliko hilo la asilimia 0.2 limechangiwa na kasi ya mabadiliko ya bidhaa za vyakula kama unga wa ngano kwa asilimia 6.8, nyama ya ng’ombe kwa asilimia 3.4, maziwa ya unga kwa asilimia 9.2, mayai kwa asilimia 5.0 na viazi mviringo kwa asilimia 4.7 na kufanya kuongezeka kwa asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.6 mwezi Agosti.
Amesema pia bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko ni gesi ya kupikia kwa asilimia 2.7, mkaa kwa asilimia 3.5, na huduma ya malazi katika nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7na kufanya bidhaa hizo kuongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.0 mwezi Agosti.
Mwananchi