OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
KINARA wa mabao wa Ligi Kuu Bara kwa msimu uliopita, George Mpole anayekipiga FC Lupopo ya DR Congo kwa sasa amesema kutinga kwa Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imeiheshimisha Tanzania na kutoa fursa kwa vijana kupata nafasi zaidi za kutoka nje ya nchi.
Simba ilipata ushindi wa mabao 7-0 juzi dhidi ya Horoya ya Guinea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kujihakikishia kwenda robo fainali ikiwa na mechi moja mkononi nyuma ya Raja Casablanca iliyokusanya pointi 13 na zitakutana Aprili Mosi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mpole alisema mafanikio ya Simba yameifanya Tanzania iendelee kutoa timu nne kwenye mashindano ya kimataifa kutokana na pointi walizozikusanya zisizoweza kufikiwa na nchi nyingine yeyote na hiyo ni heshima kubwa kwa taifa.