fiksiman
JF-Expert Member
- May 17, 2008
- 402
- 107
Jamani mwezi ndo unaelekea ukingoni, nataka kuwatonya kituko nilichokutana nacho hivi karibuni....mkanda ulikuwa hivi:
Tulikwenda kwenye kazi na wenzangu kama wanne hivi, ilikuwa maeneo ya masaki kwa mzito mmoja...(timu ya waandishi). Basi tukachapa kazi hadi majira ya jioni sana...karibia na muda wa futari. Sasa mama mwenye nyumba akauliza kama wapo waliofunga. Wote tukaonyesha vidole.
Basi adhana ilipopigwa tukasogea kwenye mkeka na vinono vikawasili. Sasa aibu ilikuja pale tulipoanza kupiga tukio. Heee, hamadi si wadau wawili wakasali rosali (wakaonyesha alama ya msalaba kwenye paji la uso kisha wakatulia kwa muda kama wanasali). Wote tushikwa na aibu maana walikuwa watu wazima.
Jamani mwezi huu!