Mfungo wa Ramadhan na Kwaresma

Mfungo wa Ramadhan na Kwaresma

Zogoo da khama

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
631
Reaction score
592
Poleni kwa mfungo wa ramadhan na kwaresma, safari hii swaumu zimeongozana, sasa ndg zangu nina swali naomba tulijadili kwa mapana yake:

Ni hivi kila ifikapo mfungo wa ramadhan taasisi mbalimbali za umma na binafsi, mabenki, watu binafsi huandaa futari au kufutulisha makundi mbalimbali kwenye hilo ni jambo la kheri,

Vipi kuhusu kwaresma mbona sijaona yakifanyika hayo ya kufuturisha shida nini? Kwaresma inafahamika na tunafunga siku 40, ila kwa umri wangu sijasikia sijui taasisi, bank au hata huko juu wameandaa futari kwa makundi maalumu.

Tujadili bila kukwadhana maana wote tumefunga
 
Hata Mimi nashangaa taasisi zote za serikali kupamba ofisi za umma na miti sijui na mayai ya Sungura Kila Krismas! Tatizo sijui Nini!
 
1. Wengi wakristo hawafungi
2. Sio wakristo wote wanakubaliana na kwaresma
3. Wakristo hawana utaratibu wa kufturu
4. Kwaresma hapo kwenye bible
Hakuna utaratibu uliowazi, sheria wala kanuni juu ya kwaresma kwenye maandiko, ni mipango tu ya waroma.
 
Mfungo wa kwa rezima sio kitu cha lazima na ndio maana hata wakristo wenyewe huwa hawautilii maanani.

Sasa hivi ni mfungo wa kwarezima lakini unaweza kuta walio funga ndani ya nchii hii hawafiki hata 1000.
 
Inawezekana kwenda kuongea na Wahadzabe bila kitoweo Cha nyama na wakakuelewa?
 
Hoja yako ni nzuri , ukweli ni kwamba huwezi kukuta hata neno futari kwa wakristo kwasababu sio mambo yao , huu ni utaratibu wa waislamu ndio maana hata jamii imejikita kwao kwenye suala la futari
 
Kuingiza ingiza udini kwenye taasisi za umma katika nchi isiyoongozwa na dini fulani ni upuuzi
 
Back
Top Bottom