Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MFUNGO WA RAMADHANI MJINI BERLIN UJERUMANI
Sijapatapo kuishi mji mgumu duniani kama Berlin na naamini hii ni sawa katika miji yote ya Ujerumani.
Kwanza ni Wajerumani wenyewe na sura zao za chuma.
Hawana tabasamu wakati wote sura zao ni za jiwe yaani, ''stone face.''
Pili Wajerumani hawaelewi kwa nini wewe hujui Kijerumani na kuhakikisha kuwa unatia juhudi ya kukijua Kijerumani hakuna tafsiri ya tangazo lolote mahali popote.
Huna njia ya mkato ila kujifunza Kijerumani.
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umenikuta Berlin.
Siku chache kabla ya mfungo nikawa nauliza msikiti wa jirani na ratiba ya sala khasa sala ya Maghrib kwa ajili ya kufungua ''muadhin.''
Sehemu niliyokuwa naishi kulikuwa na Waturuki wengi na maduka niliyokuwa nanunua mahitaji yangu yalikuwa ya Waturuki hata migahawa niliyokuwa napita kununua, ''take away,'' zangu ilikuwa migahawa ya halal.
Lugha ikawa kikwazo changu kikubwa sana kuelewana na Mturuki mwenye duka kubwa jirani yangu lakini alinielekwa kuwa nilikuwa namuuliza msikiti.
Akanielekeza mtaa wa pili tu hapo jirani kuwa upo msikiti.
Nimepita mchana wa Ramadhani kuangalia kama nitakuta sala ya jamaa.
Hakika ulikuwa msikiti na mchana wa Ramadhani lakini sikuona dalili ya watu kuingia kusali.
Nilinyongonyea kupita kiasi.
Nimeishi Ulaya na najua hali ya Mwezi wa Ramadhani mathalan London msikiti wa White Chapel, East London au Msikiti wa Finsbury Park achilia mbali msikiti wa Regents Park.
Hii misikiti yenyewe itakupa hali ya kuwa Mwezi Mtukufu umefika.
Berlin ilikuwa tofauti sana.
Nilitamani niruke nijikute nimefika Dar es Salaam Msikiti wa Mtoro nimeswali na nasubiri kusikiliza darsa za Ramadhani.
Nilirudi nyumbani nimelowa sana.
Nilijiuliza kitu gani kimenileta huku porini.
Rafiki yangu katika Take Away yangu aliponiona akajua nimefata futari akawa ananionesha, ''barbecue,'' za kunitia hamu lakini vyote vilivyokuwapo pale vilinitumbukia nyongo achilia mbali ile kunitolea chupa ya juisi kwenye jokofu lile lile ambalo ndani yake alikuwa amaweka bia za Kijerumani.
Kanitolea kila aiana ya salad nikawa nachagua kama mtu niliyepigwa na radi nachukua tu lakini moyo wangu haukuwapo katika ile futari.
Nimeadhini mwenyewe chumbani kwangu nimefungua muadhini kisha nimeswali.
Sijapatapo katika maisha yangu kushuhudia Ramadhani ya unyonge kama hii.
Hii kwa unyonge ilishinda Ramadhani yangu ya kwanza Uingereza, Cardiff miaka mingi iliyopita nikiwa bado kijana sana.
Hiyo picha hapo chini ni kituo changu cha treni nashuka hapo asubuhi kisha natembea kama robo saa hadi ofisini kwangu Zentrum Moderner Orient (ZMO) taasisi ya utafiti mfano wa University of London School of Oriental and African Studies (SOAS).
ZMO wakati wa WW II jumba hili ilipokuwa ofisi yangu lilikuwa makao ya GESTAPO.
Kusafiri ni elimu tosha.