Unaonekana ulijiandaa kupinga wakati unamsoma jamaa.Yeah nmesoma
Kumbe unakaa na wakubwa hongera! Nafikiri wewe ndio uko sehemu nzuri na sio kwamba wao wako vibaya.Ila na ukubwa wa mishahara+bonus lkn maisha yao baada ya ajira hua siyaelewi,boss mstaafu wa Tbc baada Tido kwa sasa ndio mwenyekiti wetu wa mtaa na wakubwa wengine kibao hali zao ni mdogo mdogo.
Kumbe unakaa na wakubwa hongera! Nafikiri wewe ndio uko sehemu nzuri na sio kwamba wao wako vibaya.
Mkuu asikuumize kichwa huyo bibi.Sio poyoyo mleta mada yuko sahihi labda wewe hujamwelewa.
Kiukweli ajira hamna na Wasomi ni wengi. Ukweli utabaki
Wasomi waangalie namna ya kujiajiri...anapokuwa shule asiwaze ajira awaze kutafuta pesa....
Biashara wala haihitaji uzoefu toka kwa wazazi hayo ni mawazo tu mgando....you can make your own life....
Anyway
Mimi nitawaelimisha watoto wangu kuwa usomi sio ajira wajifunze namna ya kutafuta pesa nje ya ajira. Na nitawapeleka veta.
Sent using Jamii Forums mobile app
?? Vipi umenifananisha na nani?Mkuu Graph
Ile biashara yako ya kuuza maharage kule Gairo uliishia wapi ?
Vipi kuhusu wale wanachuo wenzako mliofilisika Kule ifakara wapo wapi ?
Nauliza tu mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona mzee wa hivyo wengi wao walikuwa waadilifu sana.Hapana mzee baba huku hata majirani choka mbovu kama mimi tuko wengi balaa.
Nilikua nashangaa tu,madaraka/pesa walizoshika na maisha yao ya mtaani sio directly proportional.
Daah inawezekana aisee.Ukiona mzee wa hivyo wengi wao walikuwa waadilifu sana.
Mkuu hakuna anedanganya mtu hapa, kwa kazi unayoifanya ya kuuza dagaa umejiajiri wale usijipuuze. Kitu kimoja tambua kuna tofauti kati ya kujiajiri na kufanya biashara. Anza kufikiria kufanya biashara sasa.
Mtu aliyejiajiri huwa akitaka kuajiri atatafuta mtu anayemzidi kwa mambo mengi ili aweze kumcontrol ila anayefanya biashara principle inasema only employ people who are more inteligent than you.
Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa tuache kudanganya hapa JF! Sema kweli mimi nimebahatika kupata Elimu japo sijamaliza na katika masomo yangu nilibahatika kujaribu mambo mbali mbali. Isitoshe mimi katika mambo ya IT nipo vzr sana hasa katika upande wa sim japo sijasomea hayo mambo!
Kilinisaidia sana ni kutumia smartphone toka nipo kidato cha pilo nikawa nasoma sana mtandaoni. Ukweli n kwamba mtandaoni kuna vitu vingi sana na vyema faida. Lakini ili uvipate hivi vitu lazima uwe vzr mfukoni na kiakili pia. Hivi vitu vinahitaji device kama smartphone, laptop au desktop kaka usidanganye Watanzani.
Na nimekuja kuiva sana katika mambo hizi lipoenda chuoni nikasoma Course mbili zinazohusiana na mambo ya technology japo mimi n mwalimu kitaaluma. Ukisema Online shopping kwa Tanzania hata ile mifumo ya Malipo for Online Shopping hajawa sawa kama inavyotakiwa mkuu
Ukiangalia mifumo vingi inatakiwa ukamilishe malipo ndani ya saa 1 toka ku-order bidhaa. Na hii nina ushahidi mwanzani mwa mwaka huu nilipita mtandao fulan hivi nikaona kuna bidhaa kama frash na memory card zilikuwa zinauzwa kwa bei rahisi sana mtandaoni nikaoda bana baada ya kupokea namba malipo nigaingia zangu M-pesa nikafanya malipo. Baada ya kumaliza sms ya muamala haikuja mpaka kesho yake kucheki bidhaa haijalipiwa. Afu sikupata msaada.
Kwahiyo msiwe mnakuja kutupa mambo ya uongo hapa kaka kuna mengine tumeishayafanya. Mpaka tukaamua kurudi kupambana kwa shughuli za kawaida tu. Ila sikatai kuwa fursa hazipo zipo nyingi tu lkn n ambao tayari wana mtaji wa kutoshaa.
Unapata gunia ngapi kwa hekari?Mkuu mc gregor nilianza na mtaji mdogo sana coz nina shamba la ekari mbili tangu mwaka 2005 nilikuwa napanda mahindi ya kawaida lakini kwa sasa ninapanda mahindi ya hybrid kutoka kampuni ya seed-co arusha na pia na kodisha mashamba ya wengine;
mifuko 10@12000=120000
trekta 2eka@45000=90000
dawa ya multi afa plus,booster kitu kama 50000
jumla 260000~300000/=
kununu mahindi kutoka shambani kutegemea na msimu 36 mpaka 40 kwa gunia kuuza 60 mpaka 90 kutegemea na eneo.
Gunia moja bei gani?Mkuu Avriel inategemea na mambo haya kwanza ubora wa ardhi,uandaaji mzuri,na mbegu unayopanda.
kwa huku mimi huwa napata gunia 45 kwa heka nikitumia mbegu ya tembo au kitale kutoka kenya.
lakini kama mwaka huu nina tumbili ambayo inakomaa muda mfupi miezi 3 hapo napata 30-35 gunia kwa heka