Mgambo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili acheni kufanya biashara ya barakoa (mask)

Mgambo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili acheni kufanya biashara ya barakoa (mask)

KIMARA BRIDGE

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
262
Reaction score
270
Hivi ni kwa nini mnafanya mradi wa kitoto namna hiyo, mnawazuia raia kupita kwenye geti kama hawajavaa barakoa (hata staff ambao wanapewa na mwajiri wao nyie mnalazimisha wanunue wavae wakati wana elimu ya barakoa kuliko ninyi), na huko nje mmewaweka jamaa zenu ambao hata kutunza (kuhifadhi) barakoa hawajui na hawawezi, maana yake barakoa zinapigwa na vumbi na zinashikwa na mikono ambayo siyo salama (michafu) au kwa kuwa wanaofanya hiyo biashara ni ndugu, wake zenu, waume zenu, michepuko au ni jamaa zenu.

This is not right, halafu cha ajabu nyinyi wenyewe hamvai na mtu akishapita getini anavua na anaendelea na maisha, huko ndani hata staff wenyewe hawavai (wale ambao hawahudumii wangonjwa).

Sasa nawaambia next time nitawato bandama, mkirudia tena. (simba day, yanga day na kampeni watu nyomi la hatari lakini hakuna upuuzi wa kuuza used na barakoa chafu. Naomba mamlaka husika zichuke hatua kabla raia hawaja kinukisha. Mnaweza kuwahakikishia watu kwamba hizo barakoa siyo USED?
 
Kwanini usivae barakoa yako safi uliyonunua pharmacy au sehemu unayoiamini?

Au zile za kufua uliyo fuliwa na kunyoshewa na mkeo?

Watanzania muache kulalamika kwenye mambo madogo sana tena yanaonekana ya kijinga kabisa.
 
Kwanini usivae barakoa yako safi uliyonunua pharmacy au sehemu unayoiamini?
Au zile za kufua uliyo fuliwa na kunyoshewa na mkeo?
Watanzania muache kulalamika kwenye mambo madogo sana tena yanaonekana ya kijinga kabisa.))
hakuna aliye lalamika, unajuwa siyo wote wanapenda kuvaa barakoa, sasa usilazimishe watu wavae. ule msukumo wa kuvaa barakoa ulisha isha na ndiyo maana watu wanapuyanga bila barakoa (makanisani, misikitini, viwanja vya michezo, kwenye madaladala, kumbi za starehe na sasa kwenye makampeni) na watu wameshasahau hata bei.

Na ndiyo maana nimeandika ya kwamba ni biashara ya kitoto na ya kindezi kuvizia watu na kuwalazimisha ili upate hela, kama vipi wawatangazie uma ili kila mtu ajue anapata wapi kuliko kununua barakoa ZILIZOTTUMIKA.
 
Sikuhizi muhimbil imejaa mateja (waathirika wa madawa ya kulevya) kila kona unayopita utawakuta yaani hospital imekuwa pango la wanyang'anyi, ukifika hapo getini hata kama umebeba chakula cha mgonjwa utakumbana na maswali Tu lkn hawa mateja wanapita Tu bila tabu yeyote.

Hawa wezi wote wamehamia muhimbil kama Hadi kero
 
Mkuu mbna hujiamini hao walinzi hawana lolote sema tu wanatumia ujasiri wao na nafasi yao lakini kisheria wanakosea Sana.

Sasa nawewe inabidi ujiamini na utumie hoja za kisheria na mifano kwasababu serikali imesharuhusu mikusanyko bila barakoa kwa maana corona haipo tena.

Pia ata wanaovaa apo getini wakifika ndani wanavua so hakuna cha maana apo.

Siku nyengine waambie Mimi barakoa yangu nimeifua bdo haijakauka...kama vp mnipeleke kwa hao wakuu wenu wa kazi wakikataa unapita kiubabe kama unauweza unawapa ata na makofi mazito mawili.

Kesho wakikuona wataacha huo ujinga.
 
Wanafauata dawa methadone, ni clinic yao pale ila mwisho ni saa nne, wakishatoka kupata dawa ndipo huwa wanazurura zurura pale maeneo ya nje na sio ndani ya hospital
Sikuhizi muhimbil imejaa mateja (waathirika wa madawa ya kulevya) kila kona unayopita utawakuta yaani hospital imekuwa pango la wanyang'anyi, ukifika hapo getini hata kama umebeba chakula cha mgonjwa utakumbana na maswali Tu lkn hawa mateja wanapita Tu bila tabu yeyote.

Hawa wezi wote wamehamia muhimbil kama Hadi kero
 
Back
Top Bottom