Mganga alimwambia akinywa pombe atakufa

Mganga alimwambia akinywa pombe atakufa

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Kuna waganga wengine ni wajanja sana, yani wanacheza na psychology ya mtu.

Kuna jamaa nilisoma naye chuo alikuwa rafiki yangu sana. Miaka yote tunasoma chuo hakuwahi kunywa pombe hata tukienda kula gambe kwenye pub ya polisi ambapo tulikuwa tunanunua crate kabisa maana bei hapo zilikuwa bei rahisi kweli yeye alikuwa soda tu. Nikawa nashangaa jamaa na uchizi wote mpenda madem lakini pombe hagusi kabisa.

Jamaa miaka mitatu ikakata sikuwahi kumuona akinywa pombe. Nikaja kushangaa siku tumemaliza UE ya semister ya mwisho yani tumemaliza chuo, alipiga gambe sana. Nikaona jamaa mnywaji anakula bia, nyagi ana anazimudu kweli.

Ndipo akanipa kisa chake. Jamaa kumbe kabla ya kusoma hapo chuoni alikuwa anasoma Mzumbe. Yeye na rafiki zake wawili walikuwa wazee wa gambe sana. Wanakunywa pombe wanajiona wao ndiyo wao. Pombe zikawapelekea mpaka wa kadisco wakiwa mwaka wa tatu, yani wote watatu walidisco. Jamaa ndipo akaomba tena pale chuoni akapata akaja kusoma.

Lakini kabla ya chuo wote walipeleka kwa mganga, akawapa dawa wanywe na akawambia wakithubutu kunywa pombe watakufa. Basi ndiyo maana hakuwahi kunywa pombe. Sasa siku hiyo tumemaliza UE kumbe alimpigia kumuuliza kama anaweza kunywa kidogo.

Mganga eti akamwambia anywe lakini asilewe. 😂 😂 😂 😂 Nikajua jamaa anacheza na akili zao halafu mganga mwenyewe wa Mbagala.

Jamaa toka siku hiyo akaanza kunywa gambe kinoma. Yani ni afadhali asingeambiwa anywe asilewe. Maana mpaka leo karudi kwenye ulevi. Anapata kazi anafukuzwa, kila mara jamaa halafu ana kismati cha kazi. Alipata Wizara ya fedha, akawa akipata pesa anakunywa hadi kazini haendi.

Akapata kazi TANAPA, mpake leo sijajua nini kilimpata ila nahisi ni pombe maana ghafla niliona hana ajira. Akapata kazi Bank flani, nako akawa anakunywa mpaka kuna siku kamtukana meneja wake. Tulipotena mwaka bila kuwasiliana, nimekuja wasilaina naye kama week tatu zilizopita anaiambia alifukuzwa natafuta kibarua.

Kwakweli jamaa ni cha pombe balaa. Bora mganga asingemwambia anaweza kunywa tena.
 
Jamaa alivunja masharti ya mganga ya kucheza na psychology-a yake.

Kuna kisa nimewahi kukisikia cha mwanamke mwenye mdomo sana na alikuwa ndani ya ndoa ni vurugu kila siku.

Mwanamke akaenda kwa mganga (bibi mmoja) kueleza tatizo ni kutoelewana ndani ya ndoa na mumewe.

Yule bibi mganga kumbe akachukua mkaa akausaga na kumpa akamwambia awe anauweka mdomoni kila jioni kwa muda wa siku fulani.

Mara ndoa ikarudi kwenye ustahimilifu wake kumbe ni issue ndogo tu mwanamke alikuwa mdomo wa chiriku wamempa mkaa mradi akae kimya.

Heshima kwa wazee wa zamani (Wahenga)
 
Umenichekesha sana mkuu
 
FB_IMG_16055508761286777.jpg
 
wahenga watabaki kuwa wahenga...
 
[emoji23][emoji23][emoji23]wazee ni wazee
 
Back
Top Bottom