Mganga hajigangi

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,437
Reaction score
1,027
Jamaa mmoja alishinda bahati nasibu sh. milioni 20. Kwa sababu ya matatizo ya Blood pressure aliyokuwanayo,waendesha bahati nasibu wakaamua kumtafuta daktari ili ampe mshindi ushauri wa kisaikolojia kabla ya kutajiwa kiasi alichoshinda.

Daktari akauliza ni zawadi gani atapewa mara baada ya kumpa mshindi ushauri wa kisaikolojia?. Waendesha bahati nasibu wakamwambia, 'utapata sh.milioni 10 taslimu'. Yule daktari mara baada ya kusikia dau, alianguka chini na kupoteza fahamu papo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…