Mgao ujao wa umeme…

Upole ukizidi Sana =upumbavu
 
Ni kwanini hiyo asilimia 94 haitumiki?

Kwa sababu uzalishaji wa gesi kwenye visima vya gesi ni 6% tu ya uwezo wa bomba, pamoja ya kuwa tuna hifadhi nyingi bado huko ardhini (baharini)..

Mathalani, ni sawasawa na kujenga barabara ya njia nyingi labda nane, halafu magari yanayopita yawe machache yatumie njia moja tu, hizo nyingine saba zikisubiri magari yaongezeke...

Hivyo serikali labda ijitahidi kuongeza uzalishaji, au ijenge kiwanda cha kuchakata gesi (LNG plant), kitu ambacho nadhani wakubwa ndio wapo kwenye mishemishe hizo...
 
Tatizo la kukata umeme kwa jina la huo mgao kwani limeanza awamu gani ?

Kwa kumbukumbu zangu umeme umewahi kuwepo mgao around 2006 & 2007 hata kipindi cha nyuma kabla ya hapo.

Why does that matter?
 
Wanatayarisha mazingira ya kuiuza Tanesco, kila kitu kimepangwa, wana check box tu, It’s a coup !
Hakuna haja ya kuiuza. Serikali iondoe tuu ukiritimba wa Tanesco (level the playing field) halafu wawekezaji katika sekta ya umeme waongezeke. Ukiritimba wa TTCL ulivunjwa na makampuni binafsi ya simu yakaongezeka. Zamani ukiwa na simu nyumbani unaonekana tajiri, siku hizi mpaka watu wa vijijini wana simu. Watanzania lazima mkubali Ujamaa wa Nyerere umefeli, jaribuni sera za Ubepari.
 
Preventive Maintenance & Emergence Maintenance and Repairs kwa Miundombinu ya Tanesco ni lazima na haiepukiki. Kwa baadhi ya Maeneo Nchini yamezoeleza katika Awamu zote na kelele au Umma kuarifiwa inaendana na Hali ya Upashanaji Habari. Wananchi kwa hali hii ndio tukawa na Coping Mechanisms za Standby Generators Wabongo wakaita Miradi ya Watu kuuza Ma Generator badala ya kushukuru Suruhisho kuwa mbele yao. Mfumo wa Usambazaji Wetu wa Umeme- kutumia Nguzo za Miti kwa baadhi ya Maeneo yenye (1) Maji Maji na (2) Upepo - nguzo huoza na kuanguka kila mara- Mfano Eneo la Mkata - ni Flood Plain- linatutesa kweli kweli Wilaya ya Kilosa- Nguzo kila mara huanguka na kulazimika kuzimiwa Umeme siku 3-5 kutegemea na eneo lililopatwa na masahibu haya. Transmission Line kwa basdhi ya Maeneo inahitaji Total Overhaul . Tulitahadharishwa hili kuwa lazima lifanyike au tuachie hadi ije itokee total breakdown?
 
Interesting. Naona “chadema” mpya inazaliwa hapa. Kumbe hata “pinga pinga” huwa na zamu.

Enzi zile ukijaribu kuilinganisha Tz hata na A Kusini au Kenya ilikuwa dhambi sana. Leo hii inatarajiwa mfumo wa umeme wa Tz uwe wa viwango kama vya US au Uarabuni? Chini ya uongozi wa kifisadi wa CCM? Is that a joke?

Let’s get real. It’s still the good old CCM holding the reins. Expecting miracles would be almost sinful.
 
Kanunue simu ndogo mengine haya yamesemwa yamezoeleka kuangana nawezenu kuikataa ccm hamtaki tatzo limepandwa na ccm miaka 59 leo waweze kulipangua

Hapo kanunue simu ndogo sumsang au nokia
 
Huu ni uongo, mtambo usipofanya maintenance utakuumbua tu. Pia ilisubiri January awe waziri ili ianze kuharibika?
Pikipiki tu huwezi kuendesha mwaka mzima bila service
Kuumbuka kwenyewe si ndio huku? Kwanza system ya Luku! Sasa hii. Au una amini walikuwa wanaifanyia service kama inavyotakiwa?

Amandla...
 
Kitu chochote ili kimudu kinahitaji regular service/maintenance. Na unatakiwa uwe na source nyingine ya umeme. Kwa wenzetu wanafanya service inspotakiwa, na wakati mitambo inapofanyiwa service wananunua mahitaji yao kwa wenye surplus. Tungekuwa tumeunganisha na wa msumbiji au Zambia au Kenya wakati huu ndio tungenunua kutoka kwao.
Mimi siwaelewi watu wanaoshangaa. Mara ngapi tunaambiwa kuns sehemu hazitapata maji wiki nzima kwa sababu tunafanya service mitambo ya Ruvu Juu au Chini! Huko ulikoishi uliwahi kusikia metropolis kama Dar ina kosa maji wiki nzima kwa sababu yeyote?
Hatupaki majumba yetu, tunashindwa kufanyiq service vyo vya maofisini, madirisha yakivunjika hatuweki maji, paa zinavuja, mitaro hatuzibui mpaka mvua ifike, magari ya serikali yanashindwa kubadilisha matairi , barabara kila kukicha tunajenga upya kwa sababu tulishindwa kuziba potholes, halafu tunajifanya kushangaa kwamba Tanesco walikuwa wanaburuza mitambo bila kuifanyia service! Sisi kweli watu wa ajabu.

Amandla....
 
Hata kama una akili ndogo kweli unafikiri kabisa hii mitambo inaweza kuendeshwa bila kufanyiwa mantainance kwa miaka sita? Unafikiri mantainance mpaka umeme ukatike?
Watu wanaishi kwa ku cannibalise spares, utashangaa kuwa wanashindwa kufanya major maintenance? Hawa kama walikuwa wanajitahidi walikuwa wanabadilisha oil tu lakini ile ya kubadilisha brake fluid, grease, air filter, kucheki mfumo wa umeme n.k. walikuwa hawafanyi.

Ukitembelea ofisi zetu utakuta viti kibao vimetupwa kwa sababu alipuuza kukaza screws na allan key. Wanaenda hivyo mpaka mikono inachomoka ndipo wanapoomba wanunuliwe vipya.

Amandla...
 
Hatutaki maoni yako tunataka uhalisia
 
Wana uhakika baada ya matengenezo mgao utaisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…