Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na waraka wako mreefu huu, umesahau KJ alikuwa waziri wa mambo ya nje...Unajua kama taifa kuna kitu tunakikosa. Na inabidi wanaharakati wetu bila kuzingatia vyama, katika kila unit wachukue wawakilishi wakae chini tuweke vipaumbele kama taifa. Kuwe kuna mambo ambayo kitaifa itakuwa ni marufuku kutofauti, kwani hayajakaa kivyama bali kitaifa.
Wala isiwe ni furaha kwetu eti JK kashindwa kumaliza tatizo la umeme nasi CHADEMA au CUF tushangilie na kudhani kupitia hilo ndio tupate dhamana y kuingia Ikulu.
Tanzania yetu wasomi mbona wapo na haya yanaweza kufanyiwa kazi? ebu tubadilike jamani tuache ushabiki wa kivyama as if tunashabikia timu za mipira. Masuala ya kitaifa inabidi yasiingizwe katika siasa. Ni aibu kama taifa eti tunaacha kukomalia vipaumbele vya taifa ambavyo kila mtu bila kujali vyama vyetu kila mtu anatakiwa kuvilinda kwa nguvu zote.
Na tuwe wakweli tunapochangia, tatizo la umeme limeoneka kama vile chanzo ni JK, kitu ambacho si sahihi, matatizo yalikuwepo tena makubwa even before sema media zilinyamanzia, mimi kwetu Kigoma umeme ilikuwa ni tatizo kubwa sana toka uhuru na limekuwa solved kipindi cha JK,barabara toka uhuru kigoma ilikuwa haijaunganishwa na mikoa mingine kwa lami, kiasi kwamba kutoka Kigoma tulitumia siku3 kufika Dar very soon tutatumia siku1, sasa hivi Kigoma-Bujumbura ni chini ya masaa 4.
Kuna jamaa mmoja yeye alibahatika kufanyiwa utafiti na mtaalamu wake kuhusu uchumi wake na mtaalam akamuuliza mipango yake na jamaa akasema anaplan ya kuwakaribisha ndugu zake kuja kuishi naye, na mtaalam akamshauri kuwa jitahidi kuanzia sasa uchumi wako kila mwaka ukue kwa 10% lakini jamaa hakufanya hivyo hali ya kuwa anaendelea kuwashawishi ndugu zake kuja kukaa kwake, na baada ya miaka kadhaa huyo jamaa akawa ameondoka na mji kamkabidhi mdogo wake ambaye hakujua plan za kaka yake na mara wale ndugu zake wakawa wamekuja kwa wingi na hali ikawa mbaya sana. Swali ktk mji huo nani anapaswa kuonekana chanzo cha tatizo kati ya kaka na huyo dogo?
Wee Robot, Kikwete alisema kwenye kama kuna Mtu anaweza kushauri au kuwa na maarifa mengine basi anakukaribisha Magogoni. Robot nafikiri nenda Magogogni ukamuone yule Vasco Da Gama kabla hajaenda kwenye space
Natofautiana nawe Mr Mark, kama watanzania tunachopigia kelele si Kikwete au rais mwingine yeyote Tanzania afanye kila kitu. Kelele zetu ni serekali yetu ijenge mazingira yatakayotoa nafasi ya mawazo mbadala na hata tafiti kufanyiwa kazi, na hapa ndio lilipo tatizo sasa kwa nini tusiilaumu serekali wakati haitaki ushauri wala nini ila ni ilani tuuuuu.
Inastahili kulaumiwa kwa sababu inatulazimisha kuamini kuwa ina uwezo wa kufanya kila kitu, hebu jaribu kukumbuka ni tafiti ngapi za kitaalamu zimekuwa implemented na hii si kwa sababu za kukosa pesa bali ni kukosa vipaumbele hatimaye zote zinaishia kwenye makabati. Nikupe mfano wa karibu, upande wa upinzani ulijaribu kushauri njia mpadala kwa kushuhughulikia tatizo la umeme kilichotokea Waziri Mkuu bila hata kwanza kutafuta ushauri kwa wataalam alijibu hapo hapo hapana.
Ni lazima kwanza iwepo nafasi ya mawazo na ushauri kupokelewa ndipo unayoyazungumza yatawezekana la sivyo tutaendelea kuilaumu serekali katika failure zote zinazotokea.
Wewe unafikiri Tanesco hawana short/long term plan juu ya maendeleo ya umeme, mbona hawapewi nafasi kueleza mawazo yao kitaalam?. Ukiwauliza watakwambia waliyaona haya mapema na walikuwa na ushauri kwa serekali mapema lakini nani wa kuwasikiliza?
ya nin malumbano, yanini, hakuna umeme ni hakuna, watu leo wanalalamika ndio hao hao waliwachagua hao MaJK miaka ya nyuma.
soma iyo waraka ya sa uone kama sisi nasi tunaweza kuiga mfano huo??
Ngeleja soma apa
yajengwe mabwawa madogomadogo kabla ya power plants
kwa kuwa maji huwa mengi sana wakati wa masika hata kuleta mafuriko yenye hasara kwenye baadhi ya maeneo, ivi haiwezekani kujenga mabwawa mengine madogo madogo kabla ya mtera/nyumba ya mungu/kidatu ili kutunza maji hayo pia kwa ajili ya kucontrol mafuriko? wataalamu saidien hii ni idea tu.
Maji yaliyotumika yatumike tena.
Kwa kuwa issue ni maji kujaa kwenye dam, jee haiwezekani maji yaliyotumika kuzungusha ili turbine kufanyiwa uchakachuaji yarudi tena kwenye bwawa then yatumike tena na tena na tena? wataalam mpo??