Mgawanyo wa Madaraka ya Mihimili mitatu ya Kikatiba

Mgawanyo wa Madaraka ya Mihimili mitatu ya Kikatiba

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Dhana ya mgawanyo wa madaraka inaeleza kuwa utawala wa dola unapaswa kugawanywa katika vyombo vitatu ambavyo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Kila chombo kina majukumu tofauti na chombo kingine.

Kwa mujibu wa dhana hii, mamlaka ya Serikali ni utendaji; mamlaka ya Bunge ni kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma; na mamlaka ya Mahakama ni kutafsiri sheria na kutoa Haki. Hapa nchini, dhana hii inatajwa kwenye Ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Dhana hii inazuia chombo kimoja kutawala, kuingilia na kufanya kazi za chombo kingine. Lengo la mgawanyo wa madaraka ni kuongeza ufanisi na kuleta uwajibikaji wa vyombo vya dola.
Uhuru wa Mahakama

Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwa kila jaji au hakimu yuko huru kuamua kesi iliyopo mbele yake kwa mujibu wa sheria na ushahidi ulioletwa mbele yake, na katika kutekeleza majukumu hayo, hapaswi kuingiliwa, kushawishiwa, au kushinikizwa na mtu au chombo chochote, ikiwemo Bunge na Serikali kama inavyoelezwa katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Hivyo, dhana ya uhuru wa mahakama inaitaka mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga wala
upendeleo.

Uhuru wa Mahakama unahifadhiwa na kulindwa katika maeneo manne ambayo ni:
i) Kuzuia kuondolewa kwa Jaji au Hakimu katika ofisi bila ya sababu za msingi na bila ya kufuata
taratibu zilizowekwa hata kama kuna sababu za kumuondoa,
ii) Kuweka kinga ya kutoshtakiwa kwa Jaji au Hakimu kwa makosa yoyote, yawe ya jinai au madai
kutokana na maamuzi yake ya kimahakama aliyoyafanya,
iii) Kutopunguza au kuondoa mishahara na maslahi ya Jaji au Hakimu, na
iv) Kutokuwa na vyeo kwenye vyombo vingine vya dola au kushiriki katika shughuli za vyama vya
siasa.

Hata hivyo, ni vema ikafahamika kwamba uhuru wa mahakama sio kibali kwa jaji au hakimu kuamua kesi kwa namna anavyojisikia yeye au kwa matakwa yake.

3.5 Uhuru wa Habari na Uhuru wa Vyombo vya Habari

Uhuru wa habari una maana ya watu kuweza kuzungumza na kupashana habari na kuwa na haki ya kupata habari kutoka katika vyombo vya umma na hata binafsi ambavyo vinatekeleza wajibu wa umma. Hili lazima liende sawia na kuwa na vyombo vya habari vilivyo huru, kwa maana ya kuwa na uwezo wa kutafuta na kuandika habari na kuzisambaza kwa watu ndani na nje ya mipaka ya nchi bila ya kuingiliwa na bila ya sababu maalum na Serikali. Lengo ni kuwawezesha wananchi kufahamu namna viongozi wanavyoendesha nchi na imaye kujadili na kutoa maamuzi juu ya rasilimali za nchi

SURA YA 4
4.0 HAKI ZA BINADAMU
Haki za binadamu ni stahili alizonazo kila binadamu kwa asili ya kuwa binadamu.

4.1 Vyanzo vya Haki za Binadamu nchini Tanzania

Chanzo kikuu cha haki za binadamu nchini Tanzania ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Sambamba na Katiba, vipo vyanzo vingine vya haki za binadamu nchini, kama vile, Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009, Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Namba 9 ya mwaka 2010, Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti Ukimwi Namba 28 ya mwaka 2008, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 (R.E. 2002) a binadamu ya kimataifa na ya nzania imeisaini na kuiridhia.



 
Back
Top Bottom