Mgawanyo wa Majukumu kwa Wanandoa Husaidia Kukua Kimaisha

Mgawanyo wa Majukumu kwa Wanandoa Husaidia Kukua Kimaisha

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
439
Reaction score
736
Bila kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa, Jamii imekuwa stuck katika swala la mwanaume kufanya hivi mwanaume kufanya vile, Sipingi upande wowote ule ila ningependa Tujifunze kitu kidogo pamoja Tuangalie namna gani tunaweza Move fast kimaisha

Tuangalie aina Kuu Mbili za Mahusiano na maisha ya mahusiano kama ifuatavyo:

1. Mahusiano ya Mwenza Mmoja anakazi mwingine hana
haya huwa yanakandamiza sana wadad wengi kama kakutana na mtu ambaye hataki afanye Kazi, Basi kama Mwenza mmoja anakazi na mwingine Hana, Yule mwenye kazi anapswa kujitahisi kuhudumia familia Vyema, kwasababu inamtegemea yeye na anapaswa kupambana sanaa, Na ambaye hana awe na harakati za kutafuta Kazi ili Pamoja waweze saidiana katika majukumu... Ila kwa wale hawataki wake zao wafanye kazi basi hakikisha unamlipa wewe usilete Umang'ala wa Kitemi.

2. Mahusiano ya Wenza wenye kazi wote
Hapa sasa ipo kazi, Haya mengi huwa yana upande mmoja hauridhiki mwingine unaridhika, Kuna wale wadada wenzetu wanasema kuwa "Pesa ya mwanamke ni ya mwanamke" ndugu zangu zama za sasa tutambue Watoto wakikuwa wanahitaji kukuta msingi mzuri tusiishi kama tulivyolelewa sisi, Kama hukutokea familia tajiri jitahisi watoto wako watokee familia tajiri.. Mfano: Baba analipwa 1,000,000(Milioni moja) mama analipwa 800,000(laki nane) ya mama ikiwa ya kucha, nywele na Kuvaa yeye basi ya baba itahudumia famili, mwisho wa siku mnajikuta mnatumia kile anachopata na hamuwezi kuendelea mtakuwa kwenye level moja ya maisha na kama mtapanda basi kidogo.

Lakini Mkipenda majukumu mazuri Mfano mwenye Kipato Kidogo Basi ahakikishe Nyumbani tumekula na tunavaa tunapendeza kwenye Laki nane ya mama Atoke 400,000 kwaajili ya chakula na mavazi, Then mwenye kipato kikubwa ahakikishe wanalipa kodi, na watoto wanasoma, na pamoja baada ya hayo muangalie vipi mnaweza kuanza kuwekeza ili kuja kujenga, msisubiri mpate za kustaafu.

na sio lazima mgawanyo uwe hivyo ila mnaweza kaa kama familia na kupanga majukumu bila kumkandamiza mmoja, Naamini kwa pamoja mkiwa na ushirikiano amini mtafanikiwa kwa haraka sanaa.. tena Sanaa na mta Move fast kimaisha.

NB: Tuachane na mambo y akale hakuna mahala yalitifikiza, na ndio maana familia masiki always inakuwa masikini wakifanikiwa sana ni kununua gari ila kujenga hakuna mpaka wapate zari la mentali.. ukishajua chanzo cha umasikini na ukauchukia amini kuwa utatoboa katika maisha ya mahusiano..

Je wewe mwnajukwaa Unashauri nini au unaongezea nini?
 
Back
Top Bottom