Mgawanyo wa Wabunge wanawake wa Viti Maalum katika jicho la Sheria

Mgawanyo wa Wabunge wanawake wa Viti Maalum katika jicho la Sheria

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
234
Reaction score
390
MGAWANYO WA WABUNGE WANAWAKE WA VITI MAALUM KATIKA JICHO LA SHERIA.

Kabla ya Chama cha Siasa kupewa mgao wake wa wabunge wanawake wa Viti Maalum lazima kitimize masharti yafuatayo;

(1) Lazima chama cha siasa kiwe kimeshiriki katika uchaguzi mkuu.

(2) Lazima chama cha siasa kiwe kimepata walau asilimia 5 % ya jumla ya kura halali zote katika uchaguzi wa wabunge wa majimbo.

(3) Chama cha Siasa lazima kipendekeze kwa Tume ya Uchaguzi majina ya wanawake ambao wanagombea ubunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya chama hicho kwa mpangilio wa upendeleo (order of preference).

(3) Wanawake wanaopendekezwa na Chama cha Siasa husika lazima wajaze Fomu za Uteuzi (Fomu Na. 8) na kuziwasilisha katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na viambatanusho vyake.

(4) Chama cha siasa lazima kiwasilishe mapendekezo ya majina ya wanawake ambao wanagombea ubunge wa Viti Maalum kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika muda wa siku 30 kabla ya Uchaguzi.

(5) Chama cha siasa kitapa idadi ya wabunge wa Viti Maalum kwa kuzingatia uwiano wa jumla ya kura ambazo kimepata katika uchaguzi wa wabunge. Kwa mfano, kama Idadi ya wabunge ni 100 na NCCR-Mageuzi ikapata asilimia 7% ya kura za uchaguzi wa wabunge basi NCCR-Mageuzi itapata mgao wa wabunge 7 ambao ni sawa na asilimia 7% ya kura za uchaguzi wa wabunge.

N.B: Idadi ya wabunge wanawake wa Viti Maalum ni asilimia 40% ya wabunge wote ambao sio Viti Maalum.

🔹 N.B: Mbunge aliyepita bila kupingwa

Kwa mujibu wa Ibara ya 78 (2) (a) na (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, iwapo mbunge amepita bila kupingwa basi kura zifuatazo zitahesabiwa ni kura halali za mbunge ambaye amepita bila kupingwa;

(a) Kura za mgombea Urais lakini iwapo chama cha siasa cha mgombea ubunge ambaye amepita bila kupingwa katika Jimbo la Uchaguzi kimesimamisha mgombea Urais katika Uchaguzi wa Rais.

(b) Asilimia 51% ya watu wote ambao walijiandikisha kama wapiga kura katika jimbo la uchaguzi husika lakini iwapo tu chama cha siasa cha mgombea ubunge ambaye amepita bila kupingwa katika Jimbo la Uchaguzi hakikusimamisha mgombea Urais katika Uchaguzi wa Rais.

⛔ Msingi wa Kikatiba na Kisheria wa maelezo haya ni masharti ya sheria yafuatayo;

(1) Ibara ya 78 na 81 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977

(2) Kifungu cha 86 A cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343.

(3) Kanuni ya 70 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (G.N. No. 402 of 2020)

(4) Aya ya 10 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na Wagombea, 2020


Imeandikwa na Matojo M. Cosatta, Senior JF Member.
 
Kwa hio natarajia leo wabunge wa viti maalumu wa upinzani watakuwepo!
 
Asante sana kwa kutujengea ufahamu juu. Hata hivyo, nina hoja mbili au tatu hivi. Ukipenda unaweza kuzifafanua kwa faida ya wengine pia...

1. Kumbe, majina ya wabunge hawa (viti maalumu - wanawake) hupelekwa NEC siku 30 kabla ya tarehe ya uchaguzi. Kwa maana hiyo NEC wanayo majina ya wabunge hawa na wanaweza kuendelea na mchakato wa kuwateua kwa sasa sawasawa na idadi wanayostahili, right?

2. Kama jibu ni NDIYO katika swali hili hapo juu, je ina maana hiki kinachoendelea sasa ndani ya CHADEMA, hakiwezi kuizuia NEC kufanya uteuzi wa wabunge hawa kwa sababu ushiriki wa CHADEMA uliisha katika siku 30 za kuwasilisha majina ya wabunge hawa NEC?

3. Kama jibu ktk No. 2 hapo juu ni HAPANA, je ni ushiriki na wajibu upi wa CHADEMA wanapaswa kuutenda ktk kukamilisha mchakato wa uteuzi ktk hatua hii iliyopo sasa? Na je, kama CHADEMA watashikilia msimamo wao itaathiri vipi uhalali wa kisheria wa wabunge watakaoteuliwa bila final engagement ya chama?

Asante..
 
Katibu Mkuu wa Chadema anasema kuwa Chadema bado haijawasilisha majina.
Nadhani mbali majina ya wabunge wa viti maalum yanayo wasilishwa na chama kwa tume siku 30 kabla ya uchaguzi, huwa kuna final draft inayopelekwa na Katibu mkuu (Chadema) kwa kuzingatia vipaumbele (order of preference) walivyo jiwekea wao.

Kwa kuzingatia uzoefu wa chaguzi zilizopita nadhani pamoja na vigezo vingine kuna vigezo hivi Chadema huvitumia;

1. Wabunge wote wanawake wanao gombea majimbo hupewa kipaumbele kwenye viti maalum endapo hawatashinda kwenye majimbo, hivyo wote hujaza fomu za viti maalum.

2. Idadi ya kura za ubunge zilizopatikana eneo husika, humpa kipaumbele mbunge wa viti maalum anaye tokea eneo hilo.

Kwa kuzingatia vipaumbele hivyo hapo juu labda na vingine ambavyo sijavitaja, utaona umuhimu wa Katibu mkuu kupeleka orodha mpya inayo pendekeza wabunge wa viti maalum inayozingatia vipaumbele/vigezo baada ya uchaguzi.

Kuna wale ambao wanaweza kuwa wameshinda majimbo yao, hawa watahitajika kuondolewa kwenye orodha.

Kuna wale ambao majimbo yao yamepata kura nyingi za ubunge nao watahitaji kupata preference over others.
Kuna sababu zingine kama vifo, kujivua/kuvuliwa uanachama nk nk.
 
Ndio chama cha siasa kina hiyari ya kupeleka au kukataa kupeleka kwa tume ya uchaguzi majina ya wagombea wake wa viti maalum, Chama cha siasi hakiwezi kulazimishwa kupeleka majina ya wabunge wanawake wa viti maalum.
Walishapeleka siku 30 kabla ya uchaguzi yaani kabla ua 28 Oct 2020.
Mbona unakuwa mgumu kuelewa
 
Walishapeleka siku 30 kabla ya uchaguzi yaani kabla ua 28 Oct 2020.
Mbona unakuwa mgumu kuelewa
Chadema ohh hatujapekeka wakati walipeleka kabla ya uchaguzi mkuu wanataka kuchakachua waweke watu wao
 
Chama hupeleka majina kabla ya uchaguzi

Baada ya uchaguzi kazi inabaki ki update tu majina ya kwenda Bungeni

Usipo update baada ya uchaguzi kinachofanyika no kuchukua majina yale ya awali ambayo kwa mujibu wa Chadema wameweka kina Mdee na Bulaya na ndio sababu Bulaya kachangamkia fursa kama katiwa ndimu
Asante. Ila hamna ulazima wa chama kupeleka majina.
 
Chama hupeleka majina kabla ya uchaguzi

Baada ya uchaguzi kazi inabaki ki update tu majina ya kwenda Bungeni

Usipo update baada ya uchaguzi kinachofanyika no kuchukua majina yale ya awali ambayo kwa mujibu wa Chadema wameweka kina Mdee na Bulaya na ndio sababu Bulaya kachangamkia fursa kama katiwa ndimu
Swala ku update majina haliko kwenye sheria na halitambuliwi na sheria.
 
Back
Top Bottom