I hate the ritual of 'glass za wageni' sijui na nini! Mgeni atakachoambulia kwangu ndo size yake. The best china in the house is for me and my family and they deserve them! Inabidi uishi leo, kesho who knows!
Kuna tabia nimeikumbuka wakati naishi nyumbani kwetu(kwa baba na mama).Ilikuwa akija mgeni mama anafanya juu chini apate pesa ya kununua hata mapaja ya kuku na ikiwezekana pilau linapikwa siku hiyo na sisi watoto tunabaki tunakula ugali maharage mgeni anarundikiwa vinono kwa kweli roho ilikuwa inaniuma sana hili swala sema udogo ndio ulininyima kauli.KWA SASA NIPO KIGETOGETO ILA NIKIWA NA MJI WANGU MAALUMU HII TABIA NI MARUFUKU mwendo ni kugawana utachokikuta na huwezi kuniingiza kwenye madeni kisa we mgeni.NYIE MNALIONAJE HILI?
@Kikungu, bahati nzuri nipo na mama yangu hapa (Mnyamwezi wa Sikonge, Ipole) nimemuuliza kuhusu ukarimu wa kuachia chumba; amekataa amesema hiyo ilikuwa kwa Watusi (kumbuka unyamwezini kuna watusi wengi tu).
Ila ya kufingirizwa (kupakiwa mapaja ya mbuzi) inaendelea mpaka sasa hata kwetu!
Siku hizi kuna ugeni? akijua zipo abanduki, kashachungulia jikoni kiroba cha kilo 25, korie na mazagazaga kibao ndio anahamia kabisa.
Ugeni wa zamani kama katoka kijijini utafurahi anakuja na mazaga kibao, unga au mahindi,kuku n,k utaacha kumpikia pilau?
Kaunga wewe ni ndugu yangu kabisa,Ipole kuna wajomba zangu pale,sisi kwetu Kikungu,pale Chabutwa unaingia kushoto.
Muulize mama kama yeye ni Mnyamwezi Mkonongo.Nyamwezi inachukuliwa kama general lakini kuna Wakonongo,Wasumbwa,Wanyinyembi nk.Babu yangu alikuwa na asili ya Wakonongo na miaka mingi sana hicho kitu kilkuwepo na si babu yangu alinisimulia bali miaka mingi kidogo nilihudhulia misa ya msiba ya familly member,padre alitoa habari hii kama sehemu ya mahubiri.PM me please i wanna chart a bit about your familly if you don't mind
Jamani msiniache na mimi wa PUGE
kuna tabia nimeikumbuka wakati naishi nyumbani kwetu(kwa baba na mama).ilikuwa akija mgeni mama anafanya juu chini apate pesa ya kununua hata mapaja ya kuku na ikiwezekana pilau linapikwa siku hiyo na sisi watoto tunabaki tunakula ugali maharage mgeni anarundikiwa vinono kwa kweli roho ilikuwa inaniuma sana hili swala sema udogo ndio ulininyima kauli.kwa sasa nipo kigetogeto ila nikiwa na mji wangu maalumu hii tabia ni marufuku mwendo ni kugawana utachokikuta na huwezi kuniingiza kwenye madeni kisa we mgeni.nyie mnalionaje hili?
Jamani msiniache na mimi wa PUGE