Elections 2015 Mghwira: Nitamteua Magufuli kuwa waziri

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Karatu.

Mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira amesema akipata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa Tanzania, atamteua mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kuwa Waziri wa Ujenzi.

Mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika ya moja ya mikutano ya kampeni ya chama hicho.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni zake kwa Mkoa wa Arusha, mgombea huyo alisema Dk Magufuli ni mtendaji ndiyo maana anasisitiza kujenga madaraja na barabara kila anakokwenda.

"Kazi ya rais si kujenga barabara, sasa kwa kuwa yeye yuko vizuri katika suala la ujenzi nichagueni niwe rais wenu ili nije kumchagua aendelee kujenga barabara, kazi anayoifanya kwa ufanisi," alisisitiza.

Awali, katika mikutano aliyofanya katika majimbo ya Arumeru Magharibi, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini, mgombea huyo alisema Serikali yake ina sera mahsusi kwa ajili ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa nchini ukiwa umezungukwa na rasilimali mbalimbali.

Alisema mkoa huo pekee wenye madini ya Tanzanite nchini na duniani kwa ujumla, pia una mbuga mbalimbali za wanyama. Kwa upande wa kilimo, alisema mazao kama kahawa, maua, vitunguu maji na mbogamboga ni vipaumbele vyake.

"Tunataka Watanzania wajiwekee akiba ili tutunishe mifuko ya hifadhi ya jamii. Katika utawala wetu tunataka watu milioni tano waingie kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kipindi cha mwezi mmoja," alisema na kuongeza: "Ukiweka Sh10,000 Serikali itakuongezea Sh20,000, hivyo kila mwezi utakuwa na uhakika wa kuingiza Sh30,000," alisema.

Alisema mfumo wa maisha ya Watanzania unahitaji kufanyiwa mabadiliko na wao ndio wanaopaswa kusimamia suala hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Duh!

Hapa keshaharibu hali ya hewa kabisa. Ina maana Ayattollah Ghalghali hafai kabisa kuwa Waziri Mkuu?
 
Kama anamuona Magufuli anafaa kwa uwaziri mkuu
wakati wananchi wanamjua zaidi Magufuli kuliko yeye basi bora atangaze kujitoa hizo mbio..
anampa Magufuli nguvu zaidi...huku akijipunguzia kura
 
Yaani atamteua Rais wake JMT kuwa waziri wa ujenzi..?
Huu si utani wa ngumi. Tafadhari mtake radhi Rais mtarajiwa.
 
Duh!

Hapa keshaharibu hali ya hewa kabisa. Ina maana Ayattollah Ghalghali hafai kabisa kuwa Waziri Mkuu?

. Hivi bavicha akili kwenu hamnaga jamani.....unawezaje kurupuka kuijibu hoja wakati ata kuisoma haujasoma na ukaelewa?????.....kweli lowass aliposema atatoa elimu bure hakukosea mnaitaji sana sajiliwa kwenye mpango wa MEMKWA.kasema waziri wa ujenzi wewe unasema waziri mkuu....????!!!!
 
Haihitaji rocket science kugundua maana ya haya maneno. Hadi wagombea urais wenzake wanamuona Magufuli kuwa hafai kuwa rais.

Uwaziri ndio size yake!
 
Reactions: kdc
Duh!

Hapa keshaharibu hali ya hewa kabisa. Ina maana Ayattollah Ghalghali hafai kabisa kuwa Waziri Mkuu?

Kama anamuona Magufuli anafaa kwa uwaziri mkuu
wakati wananchi wanamjua zaidi Magufuli kuliko yeye basi bora atangaze kujitoa hizo mbio..
anampa Magufuli nguvu zaidi...huku akijipunguzia kura

Wakuu hicho ni 'kijembe', kanukuliwa akisema 'Waziri wa Ujenzi' - siyo Waziri Mkuu, re:
"Kazi ya rais si kujenga barabara, sasa kwa kuwa yeye yuko vizuri katika suala la ujenzi nichagueni niwe rais wenu ili nije kumchagua aendelee kujenga barabara, kazi anayoifanya kwa ufanisi," alisisitiza.
 
Reactions: kdc
Kama anamuona Magufuli anafaa kwa uwaziri mkuu
wakati wananchi wanamjua zaidi Magufuli kuliko yeye basi bora atangaze kujitoa hizo mbio..
anampa Magufuli nguvu zaidi...huku akijipunguzia kura

Hafai u - Waziri Mkuu huyo, anafaa ujenzi!
 
Na Lowassa atampa wizara gani.?
 
Kama anamuona Magufuli anafaa kwa uwaziri mkuu
wakati wananchi wanamjua zaidi Magufuli kuliko yeye basi bora atangaze kujitoa hizo mbio..
anampa Magufuli nguvu zaidi...huku akijipunguzia kura
Sikutegemea mtu kama wewe kukurupuka na kushidwa kusoma vizuri hoja ya Mama huyo
Ameongea hayo kumponda Magufuli mtu anayetaka kua Raisi wa Tanzania kila mara kusimama na kusema hoja ya Madaraja na barabara kwahiyo hafai na hastaili kua Raisi wa Tanzania labda huo uwaziri wa hizo barabara anazozihubiri kila Mkutano.
 
Kwa uelewa wa wastani, hiyo ni turufu kwa Magufuli.
 
Huyu mama ni shujaa sana. Haijawahi tokea mama mgombea wa Urais akazunguka mikoa mingi kama anavyofanya Anna! Hotuba zake katika jukwaa ni zaidi ya dakika 60!
 
Duh!

Hapa keshaharibu hali ya hewa kabisa. Ina maana Ayattollah Ghalghali hafai kabisa kuwa Waziri Mkuu?

Amesema atamteua kuwa waziri wa ujenzi sio waziri mkuu. Zitto ndio PM kwenye serikali ya mseto ya mama Anna E Mgwhira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…