Mgogoro kwenye mgao wa uuzaji wa nyumba

Mgogoro kwenye mgao wa uuzaji wa nyumba

big dreamer

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
399
Reaction score
1,076
Wasalaam,,

Kuna majirani zetu hapa dar es salaam wananyumba imekaa mjini kabisa,,nyumba hiyo ina thaman zaid ya mil 600,,sasa ipo hivi

Hiyo nyumba kwasasa inamilikiwa na wajukuu,,,,, aliyejenga nyumba (babu choki) alishafariki mda mrefu,,watoto wa huyo mzee choki walikuwa 6 nao walikuwa hawana tamaa so hawakuuza,,,mmoja baada ya mwingne wamefariki na wa mwisho tumezika hapa karibuni,,,sasa wamebaki wajukuu tu wa mzee choki,,sasa katika watoto wa yule mzee choki mtoto mmoja wa mwisho alikuwa na mtoto mmoja tu aitwae jomo,,,ambae yupo ktk hawa wanaotaka kuuza nyumba,,lakini watoto wengne wa mzee choki wanawatoto wa kwanza anao 4, wa pili anao 5, wa tatu anao 4 ,wa nne anao 6 wa tano anawatoto 4 na huyu wamwisho alibahatika kupata mtoto mmoja tu ndio huyo niliemtaja awali aitwae jomo,,,

Sasa jomo anasema ikiuzwa nyumba pesa igawanywe kwa kila familia ya mtoto wa mzee choki ila hawa wajukuu wengne wanasema pesa ikipatikana ijumlishe idadi ya wajukuu alafu igawanywe kwa pesa iliyopo ambapo utapata 4+5+4+6+4+1=24

Kwahyo ukichukuwa let's say mill 600 ukigawa kwa wajukuu 24 means kila mmoja atapata mil 25 ,,,,,kwa hesabu hizo jomo anakuwa anapinga yeye anasema kila familia/mtoto wa mzee choki inabidi apewe mil 100 (coz wapo 6 na kuna mtu anaoffa ya mil 600) Ambapo yeye jomo peke yake anataka akunje mfukoni mil 100 hzo kwakuwa yupo pekee kwa marehem baba yake,,,,, Asante nawasilisha kwenu wataalam wa sheria mtu saidie mawazo,,,yupi yupo sahihi ktk hawa wajukuu

Nb: majina niliyotumia sio halisi
 
Wenye Urithi sio Wajukuu ni watoto so mali itagawiwa tokana na idadi ya Watoto wa Choki alafu hao wajukuu watajuana namna ya kujibalance.. Jomo yupo sawaa
 
Sawa wakuu Asante nimewaelewa naona majibu yenu wote yapo sawa hakuna alienda against another,,,basi ngoja nizidi kumpa moyo mr jomo azidi kutafuta haki yake,,uenda ataninunulia hata Pepsi siku za ufalme wake
 
Back
Top Bottom