Mgogoro wa dini wakimbiza Mkuu wa shule, wanafunzi wa Sekondari ya Bagamoyo moani Pwani...

Mboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
1,095
Reaction score
293
Mgogoro mkubwa umeibuka katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo mkoani Pwani kati ya wanafunzi wa Kiislamu na Kikristo na kusababisha Mkuu wa Shule hiyo, Bonus Ndimbo, kuikimbia shule na familia yake kuhofia usalama wa maisha yake.

Hata hivyo habari zilizopatikana shule hapo zinaeleza kuwa mgogoro huo ulianza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi.

Wakati wa uchaguzi huo walijitokeza wagombea wawili wa nafasi ya Kilanja Mkuu wa Shule, Answal Abdul na Emmanuel Mmari ambao walikuwa wakichuana nafasi hiyo. Wote ni wanasoma kidato cha tano.

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa kampeni zilipoanza wanafunzi wa Kiislamu ambao baadhi yao ni viongozi wa msikiti uliopo shuleni hapo, walianza kumpigia kampeni mgombea wa dini yao na wa dini ya Kikristo walianza kufanya hivyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wakati kampeni zikiendelea, inadaiwa Mkuu wa Shule aliwasihi wanafunzi wa Kiislamu waache kupiga kampeni kwa kufuata misingi ya dini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salehe Mbaga, akizungumza na NIPASHE jana kwa simu, alithibisha kuwepo kwa mgogoro huo, lakini alisema hajapata taarifa za kukimbia kwa Mkuu wa Shule.

“Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi,” alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Hivi huyu kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani alipatikana vipi??Kama majibu yake mepesi kama haya yametoka kinywani mwake??Tatizo la Tanzania ni kupeana vyeo kwa kufahamiana ndio maana tunapata viongozi Dhaifu kama huyu.Badala ya kushughulikia yeye anabariki hata kuondoka kwa Mkuu wa shule Uwapi Utawala wa sheria na Uongozi bora.Naililia Tanganyika.
Haya yote yaliletwa na Udahifu wa Jakaya Kikwete na serikali yake ya Ccm ambayo inazalisha viongozi kama huyu Kamanda wa Polisi.
 

Huyo mzee ndimbo ndo ameiaribu shule amekaa kidin sana
 
ninyi wote maboya. afu mnakera kinoma,hivi mmefanya hili kuwa jukwaa la majungu ya kidini? hili ni jukwaa la watu wenye akili timamu na wahitajio kupewa habari zenye akili. UISLMU, UKRISTO;WISLAMU, UKRISTO!!!!!!!!!!!!!!!1 hakuna mada nyingine ya maana?. wote wakristo na waislam wanazingua tu,tena hawana jipya. kama vp nch hii iendeshwe bila dini tena kidkteta maisha yawe kama urusi. wote siwapendi hata kidogo coz mnakera
 
Umenena dini dini umaskini huu hamuuoni nendeni kule na dini zenu hizo naamini mungu yupo siyo dini zenu mna dini nyie tuondoleeni ujinga wenu hapa.


Nayanda.
 

dogo acha mbwembwe kasome magazeti,angalia tv,sikiliza redio hii nimesoma kwenye gazeti la Nipashe sasa hebu tufahamishe chanzo nini
 
Chanzo cha habari kinaeleza kuwa kampeni zilipoanza wanafunzi wa Kiislamu ambao baadhi yao ni viongozi wa msikiti uliopo shuleni hapo, walianza kumpigia kampeni mgombea wa dini yao na wa dini ya Kikristo walianza kufanya hivyo.


Inaelekea kuwa uongozi wa Shule haukuwa na mpangilio mzuri wa kuweza kuhakikisha kuwa Dini haziingizwi kwenye kampeni za uongozi, na kutokana na nchi yetu ilipofikia sasa kuaminiana kumeshakwisha na haya ndiyo matokeo yake. Nilivyoelewa mimi na kuwa pande zote mbili zilikuwa zinapigia kampeni watu wa dini zao.

Haya yote yaliletwa na Udahifu wa Jakaya Kikwete na serikali yake ya Ccm ambayo inazalisha viongozi kama huyu Kamanda wa Polisi.

Nadhani hapo JK anasingiziwa kwa kitu ambacho hajakifanya yeye. Watu walitakiwa washtuke pale ambapo Shule za dini za msingi na Sekondari (Seminary) zilipoanza kuota kila kona ya nchi kama uyoga!
Kwa bahati mbaya zaidi, Siku hizi siyo tena Seminary za kidini bali ni vyuo vya kati na vyuo vikuu vya kidini. Kinachotokea kwenye hiyo sekondari, na vurugi nyingine nyingi tu nchini na matokeo ya miaka mingi ya sera zaa serikali, na vyama vyote vya siasa nchini kutoliangalia suala hili kimaendeleo na kitanzania na badala yake serikali na vyama vingi vya kisiasa vikawa inatumia dini kugawanya wananchi!

Tangu Seminary zianze kuwa nyingi na kuwepo kila kona nimekuwa nawaeleza marafiki zangu na watu wengi wa karibu ambapo nchi inaelekea na cha kusikitisha ni kuwa wengi wao walikuwa hawalioni hilo kama tatizo. Mimi binafsi haiingii akilini kuona ati serikali inatoa vibali vya shule za kidini ati watu wa dini moja wasome wenyewe tu (sawa na kuruhusu ubaguzi wa kidini). Je watu hao kama hawajawahi kusoma au kuwa na marafiki wa dini nyingine si watawaona kama ni maadui tu? Ukitilia maanani vitu walivyokuwa wakifundishwa wakiwa wenyewe kwenye shule hizo? Je watafanya kazi wizara gani au shirika gani ambapo hakuna watu wa dini nyingine?

Sasa tunavuna tunachopanda!
Huweza kupanda Mchongoma ukaota mchungwa, au ukapanda ngano ukavuna mpunga!
 
Huyo mkuu wa shule atakuwa ana mtindio wa ubongo na hao wanfnz watakuwa c wazima kichwani
 
Huyo mzee ndimbo ndo ameiaribu shule amekaa kidin sana

Hivi huyo mtu alokaa kidin unamfaham au unajiropokea, kavaa vipedo? kaachia ndevu chafuchafu? anajichambia jiwe? those are hopless students, wameshafeli wanatafuta legitimacy ya kufeli
 
Punguza jazba mkuu.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hivi huyo mtu alokaa kidin unamfaham au unajiropokea, kavaa vipedo? kaachia ndevu chafuchafu? anajichambia jiwe? those are hopless students, wameshafeli wanatafuta legitimacy ya kufeli

mzaz huyo ndimbo namfaham vizur tu sijakurupuka
 
Huo wimbo wa udini umeimbwa sana na tumeshauchoka.Mna ajenda gani mnaoendelea kuuimba kila siku??
 
mzaz huyo ndimbo namfaham vizur tu sijakurupuka

Je wanafunz wenyewe hao wanaoshinda nje unawajua walivyo or you need some facts? Ili uweze kuchambua pumba na mchele!
 
Je wanafunz wenyewe hao wanaoshinda nje unawajua walivyo or you need some facts? Ili uweze kuchambua pumba na mchele!

Daah bas tufanye yapo unayojua mi siyajui ng pia yapo nayojua we huyajui ila huyo ndimbo ndo amechangia kwa kias kikubwa hyo inshu mpaka kufikia huko kwanza hajafikisha hata miaka miwili pale shule kusharise conflict kibao kwanza wanafunz wenyewe walimkataa kabla hata hajakabidhiwa shule
 
Huyo mzee ndimbo ndo ameiaribu shule amekaa kidin sana

yani mkuu ilitakiwa nikutukane lakin busara zmenizuia kufanya ivo. Humjui Ndimbo vizuri na ultakiwa ukae kimya, cjapata kuktana na mkuu wa shule makini anayeweza kumfikia Ndimbo, so nakushaur ustoe conclusion kwa usilolifaham.
 

you are a GREAT THINKER BR,
 
Alichotakiwa kufanya huyo Mkuu wa Shule ni kusimamisha huo uchaguzi indefinitely.....Amani Kwanza mambo mengine baadae....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…