Uchaguzi 2020 Mgombe Urais wa CHADEMA ayaseme pia na haya kwenye Majukwaa

Uchaguzi 2020 Mgombe Urais wa CHADEMA ayaseme pia na haya kwenye Majukwaa

Kadoda nguku

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2019
Posts
332
Reaction score
475
Yapo pia mambo ambayo wapinzani inabidi wayaweke wazi kwenye majukwaa. Tunapozungumzia wapinzani naamanisha CHADEMA na ACT-Wazalendo. Wasipoyasema sasa hawatapata tena muda wa kuyaongea baada ya uchaguzi, kwa sababu najua mara baada ya kutangazwa mshindi na kuapishwa siasa za majukwaani zitafungwa tena hadi 2025.

CHADEMA na ACT-Wazalendo wayaseme haya kwa sababu hayana Afya kwa Taifa. Zitto amebadilika sana si yule tuliye mzoea kipindi akiwa CHADEMA, sasa unafanya siasa za kweli, kwa sababu anajua yeye ndiye mwanzilishi wa ACT-Wazalendo na akifanya usnitch atakuwa anajifanyia mwenyewe.

Mambo inabidi yawekwe wazi ili watanzania wayajue mapema ni haya:

1. Magu akishinda anakwenda kubadilisha katiba na kuondoa ukomo uliopo wa miaka 10. Watu waliopo karibu na Magu ndio walio ibeba ajenda hiyo, kikubwa ni tamaa zao tu za kutaka kuendelea kula maisha kwa mrija . na wana mashaka kama akiondoka hawajui atakaye kuja atakuwaje na kama wataendelea kula bata. Huu mikakati umeshafanikiwa katika barua za awali kwa kuwaengua baadhi ya wabunge wenye misimamo kutorudi bungeni, nawataja wachache change, serukamba,Maige, n.k ambao wana misimamo mikali, lakini pia wamewaingiza watu ambao wa naweza kuwanyoshea vidole na kuwaambia tumewatoa majalalani mkumbuke kama akina babu tale, maana FA, na wengine wengi tu.

Hili lisemwe kwa nguvu zote, kwa sababu wanao mpamba na kumdanganya kwamba ngosha anapendwa ni waongo ,nchi hii hadi sasa hajatokea rais kupendwa na Watanzania kama Kikwete na hajatokea wa kuvunja rekodi yake. Kipimo kizuri cha rais kupendwa ni anapoingia madarakani awamu ya kwanza na si awamu ya pili. Kikwete awamu ya kwanzanza alipata kura asilimia 84 dhidi ya huyu 52.8 . Awamu ya kwanza ndio inaonyesha ni kwa jinsi watanzania wanakukubali ila awamu ya pili inategemea na Yale uliyoyafanya kama umegusa mioyo ya watu.

2. Watumishi wanakwenda kuweka historia tena miaka mingine 5 bila ongezeko la mishahara, hivyo kuweka historia ya miaka 10 bila nyongeza. uamuzi ni wao, mwanzo hujustify mwisho wa mtu.

3. Muundo wa muungano una kwenda kurekebishwa, hilo sitaki kulichambua sana, nawaachia wazanzibar wenyew kwa sababu sisi wananchi wa huku yote kwetu ni sasa tu.

4: Kitambulisho vya ujasiriamali vinakwenda kuboreshwa na kutungiwa sheria kila raia uwe una shughuri au huna lazima uwe nacho na price yake haitakuwa hyo tena.
 
Mataga naona wanavyoiangalia kwa mbali hii habari
 
Umesahau kikotoo kipya kwa wastaafu kinaanza mwakani.

Hahahahahahhahahaha TUTAKUFAAAA.

JAMAAA KASEMA TUMPE KURA UTUONYESHE MAAJABU
 
Huu mikakati umeshafanikiwa katika barua za awali kwa kuwaengua baadhi ya wabunge wenye misimamo kutorudi bungeni, nawataja wachache change, serukamba,Maige, n.k ambao wana misimamo mikali, lakini pia wamewaingiza watu ambao wa naweza kuwanyoshea vidole na kuwaambia tumewatoa majalalani mkumbuke kama akina babu tale, maana FA, na wengine wengi tu.
In red: Hii pointi ingekuwa na mantiki kama Juma Nkamia angepitishwa! Usilazimishe hoja.
 
Umesahau kikotoo kipya kwa wastaafu kinaanza mwakani.

Hahahahahahhahahaha TUTAKUFAAAA.

JAMAAA KASEMA TUMPE KURA UTUONYESHE MAAJABU
Watanzania ukiwaambia wanaona ni matani, wakianza kutekeleza utaona vilio. Ukiwaambia huyu jamaa ni tatizo hawaamini
 
Back
Top Bottom