Elections 2010 Mgombea auza jimbo kwa Euro 1,000

Elections 2010 Mgombea auza jimbo kwa Euro 1,000

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
302
Aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Musoma Vijijini, Michael Makenji, anashikiwa na Takukuru kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Euro 1,000 (Sh. 1,850,000) kisha kujitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Soma HAPA kwa habari zaidi.

My take: Kama tuhuma hizi ni za kweli na ikathibitika kweli amepokea kama alivyokiri mwenyewe tena kwa maandishi, Je mgombea aliyetoa hiyo rushwa ataruhusiwa kuendelea na kampeni.
 
Luteni kwa serekali hii ni jinsi wasivyotaka kupoteza majimbo hilo linawezekana wangapi wana kesi mahakamani na bado wamepitishwa kugombea?
 
yaani mtu unajivua utu wako kwa Euro 1000! anajua amekata matumaini ya watanzania wangapi kwa kiwango hicho kidogo cha pesa?

kweli kwetu njaa itatumaliza
 
Hii ni Kiboko kweli pesa ni shetani nona sasa hivi anajuta ya nini alikwenda makao makuu
 
huyu inabidi afungwe sio chini ya miaka kumi ili iwe fundisho kali kwa watu wenye tabia kama yake na akitoka wawaombe radhi wananchi wa musoma vijijini
 
Alafu wanajinadi wanapita bila kupingwa kumbe kuna ishu nyuma ya pazia dahh huyu wale kichwa kabisa
 
yaani mtu unajivua utu wako kwa Euro 1000! anajua amekata matumaini ya watanzania wangapi kwa kiwango hicho kidogo cha pesa?

kweli kwetu njaa itatumaliza
Watu hatufikirii ya kesho na kesho kutwa tunawaza ya leo tu, ni kweli kwa maisha ya kijijini ukiziangalia euro 1000 utafikiri ni nyingi lakini ukianza kuzitumia hazimalizi hata wiki. Kama ulivyosema utu wake keshauza na watu hawatamwamini tena kama walivyokuwa, kweli njaa mwanaharamu.
 
Alafu wanajinadi wanapita bila kupingwa kumbe kuna ishu nyuma ya pazia dahh huyu wale kichwa kabisa
Mimi huwa siwafagilii kabisa wanaopita bila kupingwa kwa sabau yeyote ile, nasikia huko Iringa wagombea wa NCCR karibu majimbo matatu walijitoa kwa mkupuo mmoja na kuacha majimbo matano yakiwa na wagombea wa chama kimoja pekee.

Kama nchi yetu ingekuwa na utawala wa sheria ukifuatilia lazima kutakuwa na mkono wa mtu, na hii ni kudumaza demokrasia na kutowatendea haki wananchi wa majimbo husika kwa vile watakuwa hawana choice nyingine zaidi ya kumkubali aliyewekwa pale kwa just 2mil. au kuhongwa RAV4 kama tunavyosikia.
 
Ninaweza kuhisi harakati gani zinafanyika nyuma uya mapazia sasa hivi: Takukuru watajaribu kupindisha ukweli huo watasema huyo Mkono hakutoa hizo hela na hakutuma mtu yoyote aliyetoa -- kwa maana kwamba ni watendaji wa CCM mkoani/wilayani ndo walotoa. Baadhi ya hawa watakamatwa "kuhojiwa" lakini baadaye wataachiwa na kusema kwamba ushahidi ni mgumu kujua nani aliyetoa.

Hapo fisadi Nimrod atakuwa amesevu na kupeta. Huyo mpokeaji wa Chadema naye atajazwa mapesa na kuambiwa aseme hajui ni mtu gani hasa aliyemmpa hela hizo.
 
Sahihi kabisa, nami nilikuwa na mawazo hayo. Na jitihada zote hizi ni kwa sababu tu fisadi apenye mjengoni. nani asiyemjua Mkono? Yeye ni black version kwa RA - ni watu wasioguswa na utawala wa CCM, hata wafanye madhambi gani!
 
So I was right when I suspected such things from the beginning! Nyani ngabu upo??????????
 
Bora ya huyo angalau kala nyingi hawa wanao pewa buku 2 na 5 je?
Mimi nawaona wote wapumbavu tu uwe umepewa buku 2 au euro 1000 kwa vile wote wameuza utu, utu ni utu hakuna utu expensive kuzidi utu wa mwingine. Utu wa Billgate anayelala kwenye nyumba nzuri ni sawa na utu wa mmasai anayelala kwenye kichuguu.
 
Mimi huwa siwafagilii kabisa wanaopita bila kupingwa kwa sabau yeyote ile, nasikia huko Iringa wagombea wa NCCR karibu majimbo matatu walijitoa kwa mkupuo mmoja na kuacha majimbo matano yakiwa na wagombea wa chama kimoja pekee.

Kama nchi yetu ingekuwa na utawala wa sheria ukifuatilia lazima kutakuwa na mkono wa mtu, na hii ni kudumaza demokrasia na kutowatendea haki wananchi wa majimbo husika kwa vile watakuwa hawana choice nyingine zaidi ya kumkubali aliyewekwa pale kwa just 2mil. au kuhongwa RAV4 kama tunavyosikia.

IMG_9371.JPG

Huyu ni yule mwenyekiti wa Chadema akihutubia nyasi baada ya kukisaliti chama na kujiunga na vyama 12 hapa alikuwa nazindua kampeni lakini matokeo yake hata watu 100 hawakufika siku ya uzinduzi, na inasemekana sasa hivi ana gari jipya anatembelea sijui kapewa takrima tunaomba TAKUKURU wafike hapo Iringa wamchunguze huyu mwenyekiti za zamani wa chadema.
 
Bora ya huyo angalau kala nyingi hawa wanao pewa buku 2 na 5 je?

hao wengine wanaopewa buku 2 na 5 wakauza kura angalau waweza sema hawana mamlaka na hawajui walitendalo.

huyu chama kimemuamini na amewekwa kwenye nafasi ya kuleta mabadiliko kwa wengine ili hii tabia ya kupokea buku 2 na 5 ife, yeye ndo kapokea rushwa!

labda ndio njaa haichagui ....
 
Wala sio njaa ni upumbavu tu na tamaa za watu wavivu
Sawa kabisa ni upumbavu na ujuha na ujinga, kama ni njaa basi tuyaache majambazi yaendelee kuua kwa vile na yenyewe yana njaa tena kali.
 
ccm wanatafunana. huyo aliyepita bila kupingwa aliwahi kutegewa kamtego kama hako (yaani amwage mpunga wapinzani wake wajitoe apite bila kupingwa) wakakti akigombea uenyekiti wa ccm wa mkoa lakini akashtuka kuwa takakukuru anamnyatia akajitoa kuepusha soo........... inaonekana ndo kamtego kake na sasa kanaswa, kama ytaarifa hizi ni za kweli, ataenguliwa na kuwekwa ando mwaka huu...
 
]yaani mtu unajivua utu wako kwa Euro 1000! anajua amekata matumaini ya watanzania wangapi kwa kiwango hicho kidogo cha pesa?
[/B]
kweli kwetu njaa itatumaliza

Kaka hiyo ndio chadema na watu wake wanafanana!
 
Back
Top Bottom