Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Ikiwa zimesalia saa chache kabla ya kufanyika kwa zoezi la Uchaguzi wa Serikali za mitaa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTz Kanda ya Viktoria kimetangaza kupotea kwa mgombea wa chama hicho katika kata ya Buswelu A aliyepotea kabla ya kufanya mkutano wa hadhara.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Viktoria, Ezekia Wenje amesema mgombea huyo wa kata ya Buswelu A anayefahamika kwa jina la Pastory Apolinary, jana majira ya saa saba alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mdau wa chama hicho na anataka kuwapa mchango wa kuendesha kampeni na alipoenda hakurudi tena na simu zake hazipatikani mpaka sasa.
Wenje amesema kufuatia tukio hilo chama hicho tayari kimeshatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kufahamu waliohusika katika utekaji huo.
Soma pia: Ezekiah Wenje: Siasa sio ya Kubembeleza, CCM tutaenda nao Mperampera. Ukishapiga kura linda kura