Elections 2010 Mgombea CHADEMA Nkenge ajiondoa kugombea Ubunge

Elections 2010 Mgombea CHADEMA Nkenge ajiondoa kugombea Ubunge

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
Taarifa za sasa hivi ni kuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA Bw Focas amejiondoa katika kinyanganyiro hicho hivyo kuwacha wagombea wa CCM na CUFAwali ilidaiwa kuwa focas ambaye anamiliki vifaa vya mziki alidaiwa kupandikizwa na Dk Kamala aliyebwaga na Asumpta mshama katika kura za maoni.sababu za kujiondoa nitaweka hapa muda mfupi ngoja amalize kulonga na medianatumia simu
 
huyo anaatarisha maisha yake watu hawata penda hiyo
 
Mimi ndio maana SIASA za hili bara jeusi zinanishinda kbs
 
Sababu kubwa ya kujitoa ni kuwa Chama makao makuu kimeshindwa kutoa fungu la kumwezesha kufanya kampeini badala yake amekuwa akitumia fedha zake
 
kama ripoti hii ni ya kweli, hii ni pigo kwa demokrasia nchini.
 
Kwani kwa sasa hivi NEC haijaanza kuchapisha makaratasi ya kupigia kura? Kama ni ndiyo si jina lake bado litakuwepo kwenye hizo karatasi?
 
Sababu kubwa ya kujitoa ni kuwa Chama makao makuu kimeshindwa kutoa fungu la kumwezesha kufanya kampeini badala yake amekuwa akitumia fedha zake
Nafikiri hata kugombea aliomba mwenyewe hakulazimishwa na mtu hiyo ndiyo demokrasia simlaumu waliobaki wataliendeleza libeneke, hata hivyo toka mwanzo alionyesha hali hiyo.
 
Oooooh my God!!!... Kama habari hizi ni za kweli... Tunayo safari ndefu tena ndefu isiyo na mwisho... Mhh...
 
Huyo kesha Chukua Chake Mapema.

Hao ndiyo Watanzania wa leo.

Ni wanafiki, wasaliti na wabinafsi.
 
Ni vema na haki kama ni kweli ili tubaki na wanaharakat wa kweli pekee. Ni bora kuingia bungeni na wabunge wenye nia ya dhat badala ya kufungasha msururu wa watu wenye ubinafsi. Tunamtakia usaliti mwema wenye laana ya wapiga kura wake.
 
Oooooh my God!!!... Kama habari hizi ni za kweli... Tunayo safari ndefu tena ndefu isiyo na mwisho... Mhh...

Nipo kwenye hiyo press cof,ingawa imekwishasoma magazeti ya kesho,hasa gazeti la Uhuru kwani naomba mwandishi wao kama vile anaripoti live,kwani kila wakati anapiga simukazi kweli kweli mwaka huu
 
mhhh haki i wapi huyu bwana wa chadema si alionekana kukubalika sana
 
Jamani hebu nijuzeni sheria ya uchaguzi inasema nini iwapo mgombea ubunge (hata wa urais na udiwani) atajitoa baada ya jina lake kupitishwa na NEC. Jina lake linafutwa officially na NEC? Au anajitoa tu yeye mwenyewe lakini jina lake bado linakuwepo kwenye ballot paper siku ya uchaguzi?

Nasema hivi kwani pengine hizo ballot papers zitakuwa zimeshachapwa tayari na itagharimu fedha nyingine kuchapisha upya bila ya jina lake.

Swali jingine kutokana na hilo hilo: Kama jina lake bado litakuwepo kwenye ballot pape,r jee, inakuwaje iwapo wapiga kura wa jimbo husika watamchagua -- pamoja na kujitoa kwake, anaweza akaapishwa na kuwa mbunge?
 
Back
Top Bottom