Jamani hebu nijuzeni sheria ya uchaguzi inasema nini iwapo mgombea ubunge (hata wa urais na udiwani) atajitoa baada ya jina lake kupitishwa na NEC. Jina lake linafutwa officially na NEC? Au anajitoa tu yeye mwenyewe lakini jina lake bado linakuwepo kwenye ballot paper siku ya uchaguzi?
Nasema hivi kwani pengine hizo ballot papers zitakuwa zimeshachapwa tayari na itagharimu fedha nyingine kuchapisha upya bila ya jina lake.
Swali jingine kutokana na hilo hilo: Kama jina lake bado litakuwepo kwenye ballot pape,r jee, inakuwaje iwapo wapiga kura wa jimbo husika watamchagua -- pamoja na kujitoa kwake, anaweza akaapishwa na kuwa mbunge?