Ninaendelea kusisitiza kuwa vita ya ukombozi si lelemama, Vita ya ukombozi yahitaji wanamapinduzi wa ukweli na wanaharakati wanao kubali kujitoa muhanga. Hiv Wagombea wa APPT ,SAU, CHAUSTA, NCCR MAGEUZI, NRA, JAHAZI ASILI na vyama vingine visivyo na wabunge hivyo havipati RUZUKU toka SERIKALINI wagombea hao wanapata fedha toka wapi? Gharama zao za kampeni zinagharimiwa na nani? Hivyo ni wazi wagombea wengi ktk kampeni hizi wanajitegemea kwa gharama. NDIO MAANA NASISITIZA SANA WANANCHI na WAPENDA MABADILIKO tuwachangie wagombea tunao waona ni tumaini jema kwa Taifa letu bila kujali anatoka chama gani.
Ni vyema Bwana FOCUS akawa mbunifu na mkweli wakati wa kampeni zake, kwa kuwaeleza wanaomuunga mkono kuwa kampeni zinz kwama sababu ya ukata na kuomba michango kwa wenye mapenzi mema kwake na CHAMA chake, TBC jana wameonyesha mgombea wa CHADEMA huko Njombe Bw NYAGAWA na mwisho tuliona bakuli likipitishwa ili wenye mapenzi mema na CHADEMA wachangie. Pia alionyeshwa babu mmoja akikataa katakata kuchangia kwakuwa wao CHADEMA wanaitaji kura yeye atawapa lakini sio fedha. Nimetoa ushaidi huo kuonyesha kuwa fedha ni tatizo la wagombea wengi.Ushuhuda mwingine ni wa Marehemu MB PHARES KABUYE ambaye alikuwa mwalimu mstaafu na alikuwa mbunge pekee wa TLP na katika shuhuda zake alisema alitumia usafiri wa Baiskeli na wakati mwingine kwenda kwa miguu ili kuwafikia wapiga kura na kuwaomba ridhaa yao, Bw. MREMA aliwahi kukiri kuwa Marehemu KABUYE alipambana hadi kushinda bila msaada wa Fedha toka TLP Makao Makuu.(Japo kuwa ushindi wake ulitenguliwa na mahakama) na rufaa ya Bw KABUYE ilikuwa aijasikilizwa na mahakama umauti ukamfika kwa kupata ajali mkoa wa morogoro akiwa safarini kwenda Dar) Ninachotaka kuonyesha hapa kuwa si FOCUS pekee anaye tumia gharama zake, ni wajibu wake , chama chake ngazi ya wilaya mkoa na jimbo kutafuta suluhisho na si kukimbia mapambano. KUmbuken mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la mbeya mjini ameandaa CONCERT ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni zake na za DK SLAA huyo ni mpiganaji SUGU ajakata tamaa na anaendeleza mapambano bila kuchoka sababu yeye ni SUGU.
JE, matatizo utatuliwa kwa kuyakimbia?NA SUMU ujalribiwa kwa KUIONJA? FOCUS kujitoa ni kukimbia tatizo hivyo ujatafuta suluhu maana CCM wapo na ulivyojitoa umewapa nafasi ya kuendelea kuwapo hivyo WEWE ndie tatizo kwa kujitoa na kusababisha wananchi wakose nafasi ya kuliondoa tatizo CCM jimboni mwao. Na kwa kuwa sumu haijalibiwi kwa kuionja wewe umeonja Mlungula wa CCM (SUMU) sasa ujue dhambi ya usaliti itakuandama kizazi hata kizazi maana Umetenda usaliti kwa kuthubutu kuwaonjesha SUMU wana NKENGE kwa kuiachia nafasi CCM iongoze tena kwa miaka mitano mingine. FOCUS huo ni usaliti maana ilibidi ujadiliane na chama chako na kufikia muafaka nasi kujiamulia wewe kumbuka uwamuzi wako unawanyima wana NKENGE haki ya kuchagua, usingegombea ili chadema wasimamishe mgombea mwingine na wananchi wapate haki ya kuchagua.
Wana JF na watanzania wenzangu ni vyema tukumbuke mwaka huu yatupasa kuchagua mtu na si chama hivyo huyu bwana FOCUS hatakama ni mgombea wa CHADEMA na wengi mnaamini kuwa chadema ni chama mbadala lakini ukweli ni kuwa hafai na kama angeshinda ilikuwa hatari kwa waTZ wote Kumbukeni CUF wanamgombe huko NKENGE mpimeni kama ni mzalendo na mwanamageuzi wa dhati achaguliwe bila kuangalia itikadi yake. Tunachoitaji mabadiliko CHANYA na lengo ni kuitoa CCM katika uongozi wa nchi, na lengo si CCM waondoke tu bali tunaowaingiza madarakani ni viongozi wa dhati na wazalendo kwa nchi yao? kama wagombea wa upinzani ni wababaishaji ni bora kumpa mgombea mzalendo na mpiganaji wa ufisadi na mpenda maendeleo wa CCM kuliko mwizi,fisadi na kibaraka wa CHADEMA au CUF (Wa upinzani).
Pamoja na hayo yote wana JF tukumbuke maoni yetu na kuhamasishana kwetu hakutokuwa na tija kama hatuichangii CHADEMA (VYAMA VYA UPINZANI) ili iweze kushiriki kampeni bila tatizo. Kumbukeni uchaguzi ni gharama na hoja ya FOCUS kuwa kazidiwa na gharama si ya kuibeza sana kw upande mwingine inamantiki. HAYA SHIME KUJITOA KWA FOCUS KUWE CHACHU WA WAPENDA MABADILIKO KUCHANGIA CHADEMA/CUF na WAPINZNI WENGINE ILI MAFISADI WASIPATE UPENYO WA KUJIINGINZA kulaghai wagombea kwa fedha zao kwa madai wagombea hawaletewi fedha za kampeni.