Elections 2010 Mgombea Mwenza Dr Slaa

Hivi dr salim anaogopa nini kugombea? angekuwa mgombeA UPANDE WA CHADEMA AU HATA MGOMBEA MWENZA
 

WaMzizima,

Uko spot-on ..... tiketi ya ushindi ni Dr Wilbroad Slaa na Hamad Rashid Mohamed .... hiyo combination ni kiboko. Kama ulivyoshauri, ingekuwa vema kama CUF wangekubali kumuondoa Profesa Lipumba ktk kugombea uraisi
 
Here is where that part of constitution which is unconstitutional rules. Mgombea mwenza oyeeeeeee! Mtikila can help on how to go through this paradox
Mwambie Mtikila akamsaidie Mrema na TLP yake.
 
Wachangiaji wengi wamependekeza team ya Slaa na Hamad lakini wamesahau
kuwa wote hao ni wa vyama tofauti. Sheria za vyama hairuhusu miungano ya vyama kama
ilivyo kwa nchi kama ya Kenya. Si jambo rahisi kwa Hamad ambaye ni mmoja wa
waanzilishi kwa CUF kuingia CHADEMA wakati huu tukielekea katika uchaguzi mkuu.
Kwa maoni yangu hawa CHADEMA wangetafuta mgombea mwenza mtu mwengine
ambaye ni msomi na nayekubalika katika jamii, na sidhani kwama watamkosa huko
Zanzibar kwani wapo Wazanzibari wengi tu wenye sifa na ambao hawajajitokeza katika
mambo ya siasa.
 
Hoja yako ni muafaka kabisa.Ila kwangu mimi Hamadi Rashidi ananafaa sana.He seems to be serious and more committed to the wananchi.
 
Hatujasahau kuwa ni vyama tofauti ila tunaona kuwa ideally ni 'good team'. tatizo na kikwazo ni hilo swala la vyama na tafsiri ya katiba. Technically inawezekana, Hamad akahamia Chadema kwa ajili ya uchaguzi tu...Haya ni maombi yangu kwake, basi kama wakishindwa atarudi Cuf na sidhani kama Cuf watamkatalia, labda kama Lipumba ang'ang'anie kama alivyotangaza nia yake ya kugombea na kisha kumchagua Hamad kama Mwenza wake, hatujui.
Cha msingi mi niliona kwa vile Dr Slaa ametangaza nia nia ya kugombea huu ni wakati muafaka kwa vyama vikuu vya upinzani (Cuf, Nccr, Udp,Tlp n.k) kumuunga mkono na kuwatoa wagombea wao wa urais, hii ni nadharia kwa vitendo sidhani kama watakubali, tusubiri tuone...
 
Tumain kama Watanzania hawadanganyiki tena, hata ukimwaga sumu, haitasambaa, haina mashiko tena, the wind of change is sweeping across Tanzania, Soma makala ya M.M.Mwanakijiji kwenye Tanzania Daima ya leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…