GE2025 Mgombea Ubunge (CCM) Kigoma Kusini, Nuru Kashakari aahidi kujenga kituo cha Afya kwa fedha zake mwenyewe ndani ya miezi 6 akipewa ridhaa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kigoma Kusini, Nuru Kashakari (Kandahari), ameahidi kujenga kituo cha afya ndani ya miezi sita baada ya kuapishwa, akitumia fedha zake binafsi, ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ambao kwa sasa wanalazimika kusafiri zaidi ya saa nne kufuata huduma hizo

Akizungumza katika kijiji cha Rukoma, Kata ya Igalula, 'Kandahari' aliwahimiza wananchi kumchagua yeye pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan kama Rais wa Tanzania, akisisitiza kuwa miradi mikubwa iliyotekelezwa katika jimbo hilo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais huyo ni ushahidi tosha wa maendeleo yanayoendelea kuletwa kwa wananchi wa Kigoma Kusini


Your browser is not able to display this video.


Chanzo: Azam TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…