Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Khamis Mwinjuma (Mwana FA) aliwahi kukiri kuwachukia baadhi ya watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Askari wa Jiji)

Mgambo mbona ilikuwa in kero kwa kila MTU hasa wafanyabiashara ndogondogo, pia hawakuwepo katika mfumo rasmi wa ulinzi wa nchi na mali za wananchi, zaidi tu hiyo ni sanaa kwa wakati huo yawezekana hata ni mistari aliyoiweka bila kumaanisha hao mgambo wenyewe.. Sana'a wakati mwingine haiko oneway
 
Mgambo mbona ilikuwa in kero kwa kila MTU hasa wafanyabiashara ndogondogo,
Wafanyabiashara ndogondogo walikuwa hawatii sheria za nchi bila shurti. Bila hawa mgambo watanzania wengi sana wangekufa kwa kipindupindu...
 
Mdogo wangu Infantry Soldier...

Unafiki ni jukumu zito sana ambalo wengine hulishindwa kwa kuwa wamegubikwa na ufahamu.

Kila jambo Lina wakati wake na tafsiri sahihi hupatikana kupitia muktadha na mazingira.

Wimbo huo ni wa muda gani na ni kitu gani kilikua kinaendelea kati ya Askari wa jiji na Machinga?

Pole pole mwenyewe leo kagusia Jambo Hilo kwa kusema vitambulisho vya wamachinga vimeokoa adha walizokua wakipata toka kwa mgambo.

Endelea kututandikia zile makala zetu za CIA, MOSSAD, FBI, KGB, NSA nk kwakua ndio unayoyamudu siasa achana nayo kabisa ubongo wako bado mdogo.
 
Wimbo huo ni wa muda gani na ni kitu gani kilikua kinaendelea kati ya Askari wa jiji na Machinga?
Ndio maana nimeandika kwa kusema kwamba;

...........hii pia ibaki kama kumbukumbu kwa watanzania wengine wanaojihusisha na kazi za sanaa kwamba, unapokuwa unaongea ni lazima tuwe na AKIBA YA MANENO. Usiongee kwa hasira ukanena kila kitu kwa maana haujui kesho yako...
 
Endelea kututandikia zile makala zetu za CIA, MOSSAD, FBI, KGB, NSA nk kwakua ndio unayoyamudu siasa achana nayo kabisa ubongo wako bado mdogo.
Mkuu, tangia zamani ninatambua kuwa ubongo wango bado ni mdogo. Asante sana kwa kunikumbusha boss wangu...
 
Akiba ya maneno wakati Ali address tatizo lililokuwepo vividly wakati ule? Unajua maana ya akiba ya maneno Mkuu?
 
Kila jambo Lina wakati wake na tafsiri sahihi hupatikana kupitia muktadha na mazingira.
Mwana FA alionesha chuki dhidi ya wanausalama waliokuwa wanatimiza wajibu wao jambo ambalo sio sahihi katika muktadha wa siasa...
 
Pole pole mwenyewe leo kagusia Jambo Hilo kwa kusema vitambulisho vya wamachinga vimeokoa adha walizokua wakipata toka kwa mgambo.
Haiwezekani mgambo mmoja pekee afanye jambo ovu alafu mtu aseme anawachukia askari wote wa jiji. Hii sio sahihi kabisa kisiasa (Politically Incorrect)
 
Nitaamrisha watoto wangu kila moja aite mtoto wake moja jina Magufuli Hili jina limejaa uzalendo.
 
Tundu Lissu hujui geography ya Tanzania? Kwako Chato iko nchi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…