dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,991
Hawa wagombea wachanga kama huyu wa Kigamboni waliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huku wakiamini fika kuwa ujio wa Membe ndani ya ACT Wazalendo ungekuwa mkombozi kwao na walitarajia angewainua vilivyo.
Membe hata alipokuwa Pemba na Unguja pamoja na Maalim alishindwa kabisa kutumia jukwaa lake vilivyo, mbaya zaidi Membe alishindwa kabisa kutumia ujasusi wake kuweka mgombea ubunge ndani ya jimbo analotoka.
Ilitegemewa kutokana na uzoefu wa Membe basi mgombea huyo angepita kama anateleza tu. Matokeo yake mgombea wa Chadema ndiye alionekana tishio dhidi ya Nape Nnauye wa CCM. Membe alishindwa kabisa kuhakikisha kuwa jimboni kwake anaweka mizizi.
Kiukweli Membe kawaangusha sana ACT Wazalendo, pongezi kwa CHADEMA kwa kumgundua mapema. Ona sasa imebidi Zitto Kabwe ndiye awe mhimili wa chama kwa upande wa bara. Membe haonekani popote kumnadi mgombea yeyote wa ACT au hata kwenye vyombo vya habari. Huu ni zaidi ya usaliti.