Hawa wagombea wachanga kama huyu wa Kigamboni waliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huku wakiamini fika kuwa ujio wa Membe ndani ya ACT Wazalendo ungekuwa mkombozi kwao na walitarajia angewainua vilivyo.
Membe hata alipokuwa Pemba na Unguja pamoja na Maalim alishindwa kabisa kutumia jukwaa lake vilivyo, mbaya zaidi Membe alishindwa kabisa kutumia ujasusi wake kuweka mgombea ubunge ndani ya jimbo analotoka.
Ilitegemewa kutokana na uzoefu wa Membe basi mgombea huyo angepita kama anateleza tu. Matokeo yake mgombea wa Chadema ndiye alionekana tishio dhidi ya Nape Nnauye wa CCM. Membe alishindwa kabisa kuhakikisha kuwa jimboni kwake anaweka mizizi.
Kiukweli Membe kawaangusha sana ACT Wazalendo, pongezi kwa CHADEMA kwa kumgundua mapema. Ona sasa imebidi Zitto Kabwe ndiye awe mhimili wa chama kwa upande wa bara. Membe haonekani popote kumnadi mgombea yeyote wa ACT au hata kwenye vyombo vya habari. Huu ni zaidi ya usaliti.
Siku hizi kuhama ccm kwenda upinzani sio dili tena. Lowassa ndio alifanya hilo dili liwe haramu kwahiyo sasahivi watu hawana imani na makada wa muda huko CCM wanaokuja upinzani
Siku izi kuhama ccm kwenda upinzani sio dili tena. Lowassa ndio alifanya hilo dili iwe haramu kwaio saivi watu hawana iman na makada wa muda huko ccm wanaokuja upinzani
Kwa mwenye kujua saikolojia vizuri angejua Membe alishapwaya baada ya Lissu kurudi, alihisi yeye ndo angekuwa na soko lakini aliporudi TAL, soko la membe lilishuka kama nyanya mbovu sokoni!
Kuna kitu hujui.Wanachama wa CCM ni weupe sana,yaani hawawezi kuhimili mikikimikiki.Membe huko CCM alikuwa amezoea miteremko ya bao la mkono,sasa unategemea huku upinzani ataweza kuhimili bao la ukweli?
"Kazi na bata" kwisha habari yake.
Zito afanye jitihada baada ya kuungana na Chadema ammalize Lissu kisiasa kama alivyommaliza Membe ili uchaguzi ujao kwenye anga la siasa pisiwepo na mtu wakuitwa Lissu.
"Kazi na bata" kwisha habari yake.
Zito afanye jitihada baada ya kuungana na Chadema ammalize Lissu kisiasa kama alivyommaliza Membe ili uchaguzi ujao kwenye anga la siasa pisiwepo na mtu wakuitwa Lissu.
Hii ni ndoto ya saa 12 jioni wakati shetani anarejea mwilini mwako, utasubiria sana kumuona Lisu akishuka chini mpaka uzeeke na kufariki pasipo ndoto yako ya kishetani kutimia