nsharighe
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 1,441
- 2,220
Mgombea Udiwani kupitia ACT Wazarendo kata ya Kinyerezi Ndugu Albert Nyange arudi CCM leo Tarehe 24/10/ 2020,
Tukio hilo limetokea katika kampeni za lala salama za mgombea wa CCM Kata ya Kinyerezi Bi Leah Mgitu. Ndugu Nyange alipanda jukwaa la kampeni za CCM na kuwatangazia wananchi wa kata ya Kinyerezi iliyopo wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ameamua kwa ridhaa yake kurudi CCM na kumsapoti Mgombea wa CCM Mh John Pombe Magufuli, Mbunge Bi Bonnah Kamoli na Diwani wa Kinyerezi Leah Mgitu.
Uamuzi huo wa Ndugu Nyange umetokana na mgogoro unaoendelea katika chama cha ACT Wazalendo ambao umewagawa wanachama na Wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani kupitia ACT Wazalendo.