beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Chama Cha Kijamii (CCK) kimepanga kuitisha kikao kumweka kitimoto aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho, David Mwaijojele, kutokana na kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwania nafasi hiyo
Mwaijojele ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCK, alienguliwa kuwania urais baada ya mgombea mwenza wake kutohudhuria urejeshaji wa fomu katika ofisi za tume jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Renatus Muabhi, akizungumza na Nipashe jana, alidai Mwaijojele alikuwa na uhusiano mbovu na viongozi wenzake na ndicho kiini cha kutopewa ushirikiano tangu mwanzo wa mchakato.
“Tutaitisha kikao ambacho kitahoji mwenendo mzima ulivyofanyika mpaka kukifikisha chama kwenye hatua hii, tunafahamu mchakato huu ulikuwa wa kifamilia, haukuwa na baraka za kichama,” alidai.
Akijibu tuhuma hizo, Mwaijojele alisema kuenguliwa kwake na NEC hakukutokana na kususwa na viongozi wenzake wa chama hicho.
“Wewe unafahamu masharti ya uchaguzi hasa kwa nafasi ya rais, hauwezi ukaendesha uchaguzi kifamilia, maana unakuwa na fomu 14 mikoa ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar. Sasa ni familia gani inaweza ikaenda huku bara na visiwani?” alihoji.
Mwaijojele alisema mkutano mkuu wa chama ambao pia ulihudhuriwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, ndiyo uliompitisha kuwania urais kwa kura zote.
“Kwanza, Muabhi ni mwanachama wa kawaida, siyo Katibu Mkuu wa chama, alikuwa kiongozi zamani, lakini akaondolewa kwenye nafasi hiyo kwa taratibu za chama," alisema.