Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ADC, Bi. Queen Cuthbert Sendiga apiga kura. Asema Uchaguzi ni shindano na amejiandaa kupokea matokeo

ADC Party

Member
Joined
Sep 14, 2020
Posts
28
Reaction score
29
Mgombea Urais wa JMT kupitia Chama cha ADC, Queen Cuthbert Sendiga amepiga kura katika Kituo cha Ununio jijini Dar es Salaam ambapo amesema amejiandaa kwa namna yeyote.

Amesema, "Nikishinda nitashukuru kwasababu nitapata ile fursa kubwa ambayo nimekuwa na hamu ya kuipata ili niweze kuwatumikia Watanzania. Lakini pia kama kura hazikutosha bado haiwezi kunipa sababu ya kutokuwatumikia Watanzania"

1.jpg
2.jpg
 
Tuwekee na picha basi ya Her Excellency Madam President Queen Sendiga.

Hivi ikitokea akashinda, Mume wake ataitwa jina gani vile? First Man au First Gentleman!! Hiki kidhungu hiki!! We acha tu.

Naona anapitia njia ile ile ya mtangulizi wake Mh. Anna Mghwira (RC Kilimanjaro)
 
Hahaha hawa ni washereheshaji wanafahamika.

Hawa ndio hufuata mdundiko hata hawajui sherehe iko wapi. Wakisikia ngoma wanaanza kucheza.
 
Tuwekee na picha basi ya Her Excellency Madam President Queen Sendiga.

Hivi ikitokea akashinda, Mume wake ataitwa jina gani vile? First Man au First Gentleman!! Hiki kidhungu hiki!! We acha tu.

Naona anapitia njia ile ile ya mtangulizi wake Mh. Anna Mghwira (RC Kilimanjaro)
Kidhungu wanaita First Gentleman au First Spouse.
 
Huyu mama hana tofauti na Anna Mhwira.

Naye ana ndoto za kuteuliwa hata ubalozi, ni yeye kusema tu uchaguzi ulikua huru na haki.
 
Huyu dada ni CCM damu damu tena kidole gumba akiwa anaongea huwa kiko juu juu. Jana kupitia ITV alikuwa anaomba kazi kwa chama kitakacho shinda kuwa yuko tayari kufanya kazi kama Anna yule wa ACT.
 
Hongera sana Mama Jasiri, hakika nilipenda kampeni zako za kistaarabu, zenye hoja, sera nzuri. Nakupenda mno.
 
Hongera sana Queen. Mwanamke shupavu, Akili nyingi, kampeni za kistaarabu, chama chako tuu ndio kilikua hakijajipanga kushika dola

Nadhani hutapotea kwenye medani za siasa💥👍
 
Hongera sana Queen. Mwanamke shupavu, Akili nyingi, kampeni za kistaarabu, chama chako tuu ndio kilikua hakijajipanga kushika dola

Nadhani hutapotea kwenye medani za siasa[emoji95][emoji106]
Ni mwanamke bora kuliko yule mama yenu[emoji28]

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Mgombea Urais wa JMT kupitia Chama cha ADC, Queen Cuthbert Sendiga amepiga kura katika Kituo cha Ununio jijini Dar es Salaam ambapo amesema amejiandaa kwa namna yeyote.

Amesema, "Nikishinda nitashukuru kwasababu nitapata ile fursa kubwa ambayo nimekuwa na hamu ya kuipata ili niweze kuwatumikia Watanzania. Lakini pia kama kura hazikutosha bado haiwezi kunipa sababu ya kutokuwatumikia Watanzania"

Hongera Queen Sendiga kuteuliwa RC.
Pasco
 
Back
Top Bottom