Pre GE2025 Mgombea urais NCCR Mageuzi kujulikana Aprili 30

Pre GE2025 Mgombea urais NCCR Mageuzi kujulikana Aprili 30

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Hekaheka za uchaguzi mkuu zinaendelea kushika kasi huku vyama vya siasa vikiendelea na mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi ya urais.

1740398153855.png
Kwa upande wa NCCR Mageuzi, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Utawala wa chama hicho, Florian Mbeo, akizungumza leo Jumatatu, Februari 24, 2025 na Mwananchi kwa simu, amesema baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Februari 18, 2025, iliamuliwa Aprili 30 ndiyo siku ambayo chama hicho kitamtangaza rasmi mgombea wake wa urais kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tarehe hiyo pia imepangwa kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama na miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais Jamhuri na Zanzibar. Mbeo ameongeza kuwa kikao hicho pia kiliridhia kuwa Aprili 30 itakuwa siku ya mkutano mkuu wa uchaguzi.

Soma: NCCR Mageuzi wasema hawapo tayari kuunganisha nguvu na chama chochote cha upinzani
 
Back
Top Bottom