Mgombea Urais TLS ahaidi kuondoa makundi na kuleta mshikamano

Mgombea Urais TLS ahaidi kuondoa makundi na kuleta mshikamano

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS),Shehzada Walli amehaidi kuondoa makundi na kuleta mshikamano ndani ya chama hicho ambacho ni miongoni mwa vyama vya wanataaaluma vyenye nguvu hapa nchini.

Walli alitoa kauli hiyo leo wakati akihojiwa na waandishi mbalimbali wa habari katika hoteli ya Lush Garden ambako mchakato wa uchaguzi wa chama hicho unaendelea kufanyika .

Akihojiwa na waandishi wa habari mgombea huyo alisema kwamba kazi kubwa atakayoifanya pindi atakapochaguliwa kuwa Rais wa chama hicho ni kuondoa makundi na matabaka mbalimbali ndani ya TLS.

“Lazima tuboreshe chama kiwe imara ikiwa ni pamoja na kuondoa makundi na matabaka ambayo yameibuka kama ya kisiasa hii ndio kazi kubwa nitakayokwenda kuifanya “alisema Walli

Hatahivyo,alisisitiza kwamba pindi atakapopewa ridhaa atahakikisha anatengeneza mfumo wa kuwaumganisha mawakili vijana na wale waandamizi ili waweze kushirikiana pamoja na kubadilishana ujuzi.

Mgombea huyo alisisitiza kwamba atafanya kazi kubwa ya kuwaleta mawakili waandamizi ili waweze kutoa mafunzo kwa mawakili vijana kwa kuwa asilimia kubwa kwa sasa mawakili wengi nchini ni vijana.

Waliii alisema kwamba atahakikisha TLS inaishauri serikali katika masuala ya utawala bora na kufuata sheria kama njia mojawapo ya kuwaunganisha wananchi na serikali katika kuleta haki na usawa kwa kila mtu.

“Lazima tupate mtu atakayeishauri serikali katika masuala ya utawala bora na kufuata sheria na huyo mtu ni mimi pekee “alisema Walli

Naye Ipilinga Panya ambaye ni mjumbe katika uchaguzi huo alisema kwamba TLS inapaswa kumchagua mgombea ambaye sera zake zitagusa makundi ya mawakili waandamizi,vijana pamoja na wanawake.

Mjumbe huyo alimpigia chapuo Walli na kusema kwamba mgombea huyo ndiye pekee hana makundi na makandokando mpaka sasa na hivyo anastahili kuchaguliwa.

“Walli anatosha kukiunganisha chama na serikali lazima tumpate Rais kijana ambaye hana makundi wala kashfa “alisema Panya

Uchaguzi wa TLS unataraji kufanyika keshokutwa jijini Arusha ambapo mpaka sasa mchuano mkali unaendelea kwa baadhi ya wagombea wa nafasi ya urais ambao ni Edward Hoseah,Francis Stolla,Albert Msando na Flaviana Charles.

Mwisho

Pichani chini mgombea wa nafasi ya urais ndani ya TLS,Shehzada Walli picha nyingine ni mpambe wake,Ipilinga Panya

802623FF-06F4-4EE1-B6DE-5332E3424133.jpeg


378D5965-20A2-42E8-9A65-1A5072BE5B3E.jpeg


142DE207-CAB0-4634-BD47-7E78AF071DDF.jpeg


D58F5E39-DC96-40ED-99DA-AFA260634820.jpeg
 
Back
Top Bottom