ADC Party
Member
- Sep 14, 2020
- 28
- 29
Mgombea wa kiti cha Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADC, Bi Queen Cuthbert Sendiga ameendelea na kampeni zake leo katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo.
Leo hii mapema akiwa katika viwanja vya oko la Samaki aliweza kuelezea vipaumbele vyake 3 ambavyo vipo ndani ya Ilani hasa akigusia katika sekta ya Uvuvi alisema haya:
"Wavuvi ni kundi kubwa sana ambalo ukiwatengenezea maisha mazuri, mipango na taratibu tunatengeneza ajira nyingi sana za kutosha na zenye uhakika badala ya kwamba mvuvi akiumwa siku tatu ama siku nne hawezi kwenda kuvua tena sababu hakuna uwezo wa kuweka akiba.
“Chama cha ADC chini ya uongozi wangu kwa miaka mitano tunaenda kuhakikisha mvuvi wa kitanzania anaenda kua mvuvi bora, mwenye kupatiwa elimu juu ya shughuli zake za uvuvi, mwenye kupatiwa vitendea kazi bora na kuondolewa tozo zisizoendana na uwezo wake wa kuvua, na cha mwisho anaenda kuongezewa thamani ya bidhaa zake zinazotoka baharini ili iweze kumkwamua kutoka alipo kimaisha "
PICHA: Mgombea wa Urais kupitia ADC akiongea na wananchi, wavuvi na wafanyabiashara wa Soko la Samaki huko Bagamoyo mapema leo Jumamosi, Septemba 3, 2020 👇🏾