CCM ina matatizo zaidi ya mawili.
Mosi tatizo la ajira hasa vijana wengi wamekata tamaa wanajua pasipo shaka yoyote aliyesababisha tatizo lao ni CCM.
Pili huduma mbovu za afya hasa wazee,mama na mtoto hawana uhakika wa huduma bora,madawa na vifaa tiba.Tumeshuhudia kina mama watatu hadi wanne wakilala kitanda kimoja kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua.
Tatu ahadi za uongo zimekuwa nyingi sana kiasi wananchi wemechoka kudanganywa.
Nne CCM imejaa kibri,imekuwa ikitumia majory mjengoni kupitisha mambo ya hovyo bahati mbaya luninga zinaonyesha madudu yote.
Tano Watanzania walitoa maoni kuhusu katiba ya nchi mambo yote ya msingi yameondolewa na wabunge/wajumbe wa CCM.
Sita CCM imeharibu uchumi wa nchi,deni la taifa limekuwa kubwa mno,mfumuko wa bei umekuwa wa kutisha,thamani ya fedha yetu imeshuka kupita kiasi.
Saba viwanda vingi vilivyojengwa enzi za utawala wa Mwl Nyerere vimekufa au vimeuliwa maksudi na serekali ya CCM matokeo yake ni kusababisha ukosefu mkubwa wa ajira.