beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mgombea urais kupitia Chama cha Democratic (DP), Philipo Fumbo, amesema wananchi wakikipa chama hicho ridhaa kushika madaraka, serikali yake itatoa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili ili viweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Akizungumza jana katika mahojiano maalum na gazeti hili, alisema utaratibu wa kutoa ruzuku kwa ubaguzi ndiyo umefanya baadhi ya vyama kushindwa kuanza kampeni kwa wakati kwa sababu havina pesa.
"Leo unatunyima ruzuku sisi DP wakati chama chetu kimesajiliwa tangu mwaka 2002, haya ni maajabu kabisa, serikali yangu nitakayoiongoza itatoa ruzuku kwa vyama vyote bila kubagua,” alisema.
Alisema ruzuku hiyo itatolewa kwa makundi mawili, kundi la kwanza itakuwa sawa sawa kwa vyama vyote vyenye usajili wa kudumu ili kuonyesha usawa kwa vyama vyote.
Fumbo alisema ruzuku ya pili itatolewa kutokana na uwingi na idadi ya kura, na hakuna kura itakayokosa ruzuku hata kama chama kimepata kura mbili.
“Hii ndiyo itakayokuwa misingi ya demokrasia ya kujenga chama, lakini leo vyama vinapokea ruzuku na vingine havipokei, wakati vingine havina muda mrefu tangu vimeanzishwa, hiki ni kiini macho cha demokrasia,” alisema.
Aliongeza kuwa mambo mengine ambayo serikali yake itayawekea mkazo ni rasilimali ya nchi kumilikiwa na wazawa.
“Hatuna maana kwamba tutawafukuza wawekezaji wa nje la hasha, tutakachokifanya uwekezaji wowote wazawa ndio watakaopewa kipaumbele, ukija wewe mwekezaji kutoka nje lazima wazawa wawe na hisa utakavyowekeza,” alisema.
Kuhusu elimu alisema serikali yake itahakikisha inatoa mahitaji yote ya muhimu kwa wanafunzi kama kalamu, sare, na elimu itakuwa ni bure.
Kwa wanafunzi watakaofaulu kwenda kusoma katika shule za vipaji maalum, serikali itawapa vibali maalum vya kusafiri bure.
Kuhusu kilimo, alisema chama chake kinaamini ndio uti wa mgongo, lakini kilimo cha sasa imebaki ni kiini macho miaka sitini sasa ya uhuru, pembejeo zinachelewa kufika kwa wakulima kwa wakati.
Alisema serikali yake itaweka trekta katika kila ofisi ya serikali ya kijiji ambapo mwananchi akishathibitishwa kwamba huyu ameandaa shamba lake vizuri, atachangia shilingi 20,000 tu na gharama zingine zitachangiwa na serikali.
Katika sekta ya afya, alisema kwa sasa imekuwa ni changamoto kutokana na vitendo vya aibu na maiti kuzuiliwa kutokana na kudaiwa gharama za matibabu.
Alisema serikali yake itaweka utaratibu ambao mtu akishafariki hakuna tena ndugu ama jamaa kuanza kudaiwa gharama alizotumia wakati akipatiwa akiwa hospitali.
IPP MEDIA