Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Mgombea huyo, Philipo John Fumbo akiwa Uvinza mkoani Kigoma hivi sasa katika kampeni amelalamikia suala la uwezeshwaji wa Wagombea na ofisi ya msajili.
Amesema kuwa vyama visivyo na Wabunge vinateseka kwani Ofisi ya Msajili huendelea kutoa ruzuku kwa vyama vyenye Wabunge hata baada ya Bunge kuvunjwa badala ya kugawa fedha kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi.
Ameongeza kuwa hii hupelekea changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa posho kwa waandishi na hivyo kushindwa kupata nafasi ya kusikika kwenye vyombo vya habari.
Aidha, ameeleza changamoto ya ukosefu wa nauli za kuwafikisha mawakala wa vyama maeneo ya kuapishwa inayopelekea kukosa mawakala kwa vituo vingi nchi nzima.