Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha UPDP, Twalib Ibrahim Kadege amefika katika Ofisi za NEC kuchukua fomu

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha UPDP, Twalib Ibrahim Kadege amefika katika Ofisi za NEC kuchukua fomu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mgombea wa Chama cha UPDP, Twalib Ibrahim Kadege amefika katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7, 2020 kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania.

Amefika katika Ofisi hizo na Mgombea Mwenza, Ramadhan Ally Abdallah na wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage.

Chama hicho kimekuwa cha saba kuchukua fomu. Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi Agosti 25, 2020.

photo_2020-08-07_13-24-38.jpg
 
Back
Top Bottom