Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mgombea Uenyekiti wa Kijiji cha Ilula, Kata ya Ilula, Jimbo la Kwimba, Silvester Cherehani amesikitishwa kuona watu wa kijiji hicho wakipata misukosuko kwa sababu ya kuuliza mapato na matumizi ya kijiji.
Amesema "Kuna vitisho vingi. Hapa ukiuliza fedha. Unawekwa ndani. Naomba ndugu zangu nitumeni nikafanye hiyo kazi."
Naye Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Bara, Ester Thomas amemkabidhi Mzee Cherehani Ilani ya ACT Wazalendo ya Uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji wakati wa uzinduzi wa kampeni, Novemba 20, 2024.