Uchaguzi 2020 Mgombea wa ADC afanya kampeni Dar, asisitiza suala la amani kuelekea Oktoba 28

Uchaguzi 2020 Mgombea wa ADC afanya kampeni Dar, asisitiza suala la amani kuelekea Oktoba 28

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Queen Cuthbert Sendiga ameendelea na kampeni zake leo Jijini Dar es salaam katika wilaya ya Kinondoni, huku akitumia fursa ya kuwafikia wafanyabiashara na wajasiriamali katika maeneo yao husika na kuweka kuwaelezea sera na vipaumbele vyake.

Aidha, Mgombea huyo amesisitiza suala la wananchi na wakazi wa Ununio vilevile Kawe juu ya kuitunza amani ya nchi yetu kwa hali na mali hasa katika kipindi hiki cha Uhaguzi Mkuu kuelekea tarehe 28 Oktoba, amewaomba waweze kumpigia kura ya ndio kwakuwa ana uwezo mkubwa wa kwenda kusimamia mifumo mizuri ya kuipeleka Tanzania katika maendeleo yatakayomgusa Mtanzania moja kwa moja. Kesho ataendelea na kampeni zake katika wilaya ya Temeke.

0A20A305-4E63-4E5F-B252-90F79FB29BDC.jpeg
890248B0-9113-47AB-9334-2A4E52779BA8.jpeg
9163AAEF-113A-4FFC-91B6-0203900D3316.jpeg
 
Back
Top Bottom