Mwanaume aliyenukuliwa katika kipande kifupi cha video kwa kauli yake tata kuhusu jinsia yake baada ya kudai kuwa yeye ni mwanamke, licha ya kuwa ni mwanaume kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi huko Makate, ametoa ufafanuzi.
Eston Chaula amedai kuwa hakuwa na lengo baya na kauli yake bali alisimama kumwakilisha binti yake Roska Chaula ambaye hakuwepo muda huo, alikuwa amesafiri kwa ajili kwenda kumuona mgonjwa huko Mbeya