Elections 2010 Mgombea wa CCM apata wakati mgumu Musoma

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239


Habari zilizoingia kwangu jioni hii ni kwamba Mgombea ubunge wa CCM wa Musoma Mjini Vedasto Maninyi leo saa kumi jioni amekaribishwa kwa mawe na wanafunzi wa Sekondari ya Musoma alipojipeleka pale kunadi sera zake. Ilibidi aondoke haraka yeye na wapambe wake bila kuhutubia mtu yoyote.


Wanafunzi walisikika wakisema hapa anaingia Dr wa ukweli tu, au wagombea wa chama chake na si sura nyingine yoyote Hizi habari ni za uhakika kabisa.




 
:nono:nafikiri mawe si sawa nawashauri hao vijana wa shule wawe waungwana kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa au uelewa japo kidogo. wangemwonyesha ishara ya chama yaani vidole viwili hewani vurugu si nzuri tutunze amani yetu ambayo ni lulu dunia nzima,
mungu ibariki Tanzania
 
patience has its limits....

Hizi kampeni zingeendelea kwa wiki mbili zaidi nahisi pasingetosha. Kadiri siku zinavyoyoyoma naona ma uvumilivu unawashinda watu.
 
Kurusha mawe ni kukomaa kwa akili, utawaambia nini wanafunzi mnaowajengea vyoo tundu 4 milion 700, mawe ni dawa ya mafisadi yaliyokomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nimependa maneno haya "hapa anaingia Dr wa ukweli tu", ila tuzuie jazba zetu waungwana. 31 tukamkabidhi nchi Dr wa ukweli "Slaa" kwa amani.
 
Niwajuavyo hao boys, ni wanaume wala si wa kiume!
 
Nakuunga mkono mkuu, tusiwe tusiosikia, Dr. wa ukweli kasema tuwaache tu ila tu siku ya kura tufanye kweli
 
Hiyo ndo new blood. Haiwezi kudanganywa na sera mbovu za CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…