Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 11,936
- 15,196
Wandugu kwema?
Ukishangaa ya musa utayaona ya firauni. Hivi ndivyo unaweza kusema. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mgombea nafasi ya uwenyekiti kupitia CCM bwana ABDALLA KIBELE jana alionekana mitaani akiwa ameambatana na wapiga MDUNDIKO.
Mgombea huyo hakuwa anaongea lolote kwa wananchi kwa maana ya kuinadi hiyo inayoitwa ILANI Ya chama chake endapo atachaguliwa, badala yake bwana Kibele aliongozana na ma mama yaliyovalia nguo za chama huku yakinengua na kukata mauno bila soni kama hayawani.
Kitendo cha mgombea huyu bwana ABDALLA KIBELE Kupita na MDUNDIKO bila kunadi ilani ya chama chake kimechukuliwa kama DHARAU na DHIHAKA dhidi ya wapiga kura ambao wengi wanajiuliza
1. Hivi huyu bwana ABDALLA KIBELE mgombea anatuchkuliaje sisi wakazi wa KUNDUCHI?
2. Kwamba pamoja na changamoto zote zinazotukabili ikiwemo ulinzi na usalama [ pamekuwepo na wizi katika maeneo mengi ya Kunduchi haswa maeneo ya pwani], uchafu wa mazingira na ubovu wa miundombinu hasa maeneo ya MECCO inakuaje mgombea anapita na kupiga ngoma tu bila kuahidi namna atakabiliana na hizi changamoto akishirikiana na wananchi?
3. Ni zaidi ya miezi mitatu sasa maeneo ya KUNDUCHI hasa MECCO maji hayatoki kwa uhakika, mara chache hutoka usiku wa manane tena kidogo sana. Mabomba yameota kutu kabisa na wananchi wanataabika kwa kuchota maji mbaali (Kisima cha madrasa). Wananchi wanahoji, pamoja na kwamba hakuna taarifa za kwanini hasa maji hayatoki ( mwanzo walisema kuna mabomba yamekatwa kwa ujenzi wa mwendo kasi) jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote. Inakuaje mgombea anapita na MDUNDIKO mitaani bila kuahidi chochote dhidi ya kadhia hii.
4. Elimu, yapata kama miezi mine sasa tangu bwana KIBELE Na mshirika wake Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni naibu Meya wa KINONDONI watangaze ujenzi wa shule ya msingi pale eneo la MECCO karibu na lilipokuwa Karasha la kusagia kokoto. Mpaka leo haķuna kinachoendelea kwenye ujenzi huo zaidi ya kuwekwa bango tu, huku ukibaki takribani mwezi mmoja shule kufunguliwa. Itakumbukwa watoto wa salasala, mtalu ona na maeneo yote ya MECCO wanalazimika kutembea zaidi ya km 2 mpaka 3 kwenda shuleni MTONGANI na MTAKUJA.
Wananchi wanahoji licha ya kuwepo kwa changamoto hii ya watoto kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu. Inakuwaje mwenyekiti mtarajiwa bwana ABDALLA KIBELE anapita mitaani na VIGOMA bila kuahidi chochote juu ya namna ya kumaliza kadhia hii kwa watoto wao wanaogongwa kila siku na magari na bodaboda wakati wa kwenda na kurudi shule? Hozi ngoma ndio zitatatua changamoto hizi na nyingine? Kama siyo dharau kwa wapiga kura nini basi? Kwamba sina cha kuwambia kwani mimi ndo mimi na watake wasitake watanichagua. Hii ni dharau na dhihaka kwa wapiga kura wa KUNDUCHI na viunga vyake.
Kwa vyovyote iwavyo bwana ABDALLA KIBELE Hata kuwa na jambo jipya kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake kama LUSISI aliyeishia kujilimbikizia mali yeye na watoto wake. na Marehemu TABU ATHMANI ambaye naye ameishia kujitajirisha yeye na familia yake hata mauti yalipomkuta miaka mitatu iliyopita.
Mgombea huyu amekuwa na tabia ya KUWAITA WATU kwa ngoma mfano. Wakati wa mchakato kabla ya kura za maoni ndani ya chama chake. Alimualika Mzee Yusuph (yule muiimbaji na mnenguaji wa taarabu aliyekuwa maarufu) bwana ABDALLA KIBELE alimualika Mwanamuziki huyo kwa kile alichokiita kuazimisha siku yake ya KUZALIWA kumbe ni kampeni tu, wenye jicho la tatu waliona na kugundua hilo mapema kabisa sasa wakati wa kampeni anapita tena na MDUNDIKO na VIGODORO huku mitaani kwetu. Kana kwamba kero zetu zitatatuliwa na MDUNDIKO.
5. Migogoro ya ARDHI. Wakaazi wa MECCO VS SERIKALI. pamekuwepo na Migogoro mingi ya Ardhi isiiyoisha eneo la KUNDUCHI. kutaja tu michache ni mgogoro uliopo kati ya wana MECCO na Serikali. Diwani wa kata ya KUNDUCHI Bwana MICHAEL URIO akishirikiana na wana CCM wenzake (anatajwa mtoto mmoja wa kigogo) ambaye sasa ni waziri wanataka kupora ardhi ya wananchi wa eneo la MECCO waliuze kwa wawekezaji ( wao wanasingizia kwamba itakuwa katakana ya mabasi yaendayo kwa haraka) kumbe siyo kweli ni ghiriba za bwana MICHAEL URIO akishirikiana na MANYANG'AU wenzake ndani ya CCM. Licha ya kuwa wananchi wale wameshinda ile kesi lakini URIO na wenzake wamekata rufaa ili wapore lile eneo. Badala ya kuwahidi wananchi namna ya kushirikiana nao ili kutatua changamoto hii na nyingine mgombea wa CCM bwana ABDALLA KIBELE anapita na VIGOMA VYA VIGODORO na MDUNDIKO Mtaani bila kuwahidi chochote kana kwamba MDUNDIKO ndiyo utakaotatua matatizo yao
6. Kukatika kwa umeme mara kwa mara. Pamekuwepo na kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo ya KUNDUCHI wakati mwingine hata mara 4 kwa siku huku sababu zikiwa hazijulikani, itakumbukwa umeme una toa ajira nyingi kwa watu wengi hasa wafanya biashara. Badala ya kuahidi namna ya kushirikiana na wananchi kumaliza changamoto hii bwana ABDALLA KIBELE Mgombea wa CCM anakuja na MDUNDIKO bila kuongea chochote huku akigawa vipeperushi vyake vya kampeni kwa kila aliyehitaji.
7. Ukosefu wa HUDUMA ZA AFYA, Kutoka MECCO kwenda MTONGANI ilipo zahanati ya serikali pana umbali mrefu sana kama ilivyo shule msingi na secondary. Ni ngumu kwa wagonjwa kina mama na watoto hasa wajawazito kufika kule kupata huduma hii muhimu . Ni wakati sasa wa wananchi wa maeneo hayo kuwa na zahanati maeneo ya karibu. Wanayo kila sababu ya kupata huduma hii hasa ukizingatia umbali na wingi wa watu kwenye eneo husika. Badala ya kujadiliana na wananchi namna atakqvypshirikiana nao kumaliza changamoto hii bwana ABDALLA KIBELE Kibele ana pita na MDUNDIKO huku mitaani bila kunadi ilani ya chama chake? MDUNDIKO una nini cha kufanya juu ya afya na uhai wa watu hawa masikini wa KUNDUCHI?
8. Ubovu wa barabara na uchafu wa mazingira. Barabara haswa zile za mitaani ni mbovu sana hata ya kwenda ofisini kwake ni mbovu ina mashimo kama mahanadi. MECCO, JIWE GUMU, MTALU ONA na maeneo ya KWA NABII FROLA hali ya barabara ni mbovu sana hazijawahi kuchongwa wala kuwekwa lami tangu paumbwe, wakati wa mvua hujaa maji na kupitika kwa tabu sana. Mabomba ya maji yanapasuka na kuvujisha maji hovyo hali inayopelekea kuharibika kwa barabara. Mgari ya Kuzolea taka ya manispaa hayafiki kabisa maeneo hayo hivyo takataka zinasambaa kila kichochoro.
Badala ya kuahidi atafanya nn juu ya jambo hili yeye mgombea wa CCM bwana ABDALLA KIBELE Anatupigia NGOMA ZA MDUNDIKO tu kisha anagawa vipeeperushi anaondoka. Ikumbukwe bwana ABDALLA KIBELE alipita bila kupingwa baada ya CCM kuwawekea mapingamizi wagombea wengine kutoka vyama vingine kwa mizengwe. Yule wa CHADEMA aliambiwa nafasi (aliyotaka kugombea) haipo! Yaani mtu atoke kwake, akachukue fomu kisha ajaze nafasi ambayo haipo? Siyo kweli hata kidogo. Wito wangu kwa WANA KUNDUCHI.
Wakati wa kufanywa WAJINGA na WAPUUZI sasa baasi. Mtu anayekupigia MDUNDIKO bila kuahidi atafanya nni ukimchqua anakuchukulia POA na USIYEJIELEWA hivyo huna budi kumkataa kwa kumuonesha kwamba unajielewa. Kataa kunuliwa kwa MDUNDIKO. Huu ni ULAGHAI.
KURA YAKO MAENDELEO YAKO SIYO TAARABU WALA MDUNDIKO NA VIGODORO