habar wanajf,kwa anayefaham hatma ya wanafunz kada za afya kiu atujuze.
=============================
=============================
=============================
=============================
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kilichopo Gongolamboto jana waliwasilisha malalalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi baada ya kufanya mgomo kwa vipindi tofauti bila kupata majibu.
Mamia ya wanafunzi hao walifika katika ofisi ya mkuu wa mkoa saa 6 mchana kwa lengo la kupeleka kilio chao kwa Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik hata hivyo waligonga mwamba kwa kushindwa kuonana naye.
Baada ya kukosekana kwa Sadik, ilimlazimu DC Mushi, kutoka ofisi kwake na kwenda kusikiliza kilio cha wanafunzi hao.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza anayechukua Shahada ya Sayansi katika chuo hicho, Jackson Raymond, alisema kuwa wanafunzi hao wana hoja takribani 15 katika mkutano huo baina yao na mkuu huyo wa wilaya.
Alisema wanafunzi waliomaliza kozi mbalimbali katika chuo hicho wamekua hawatambuliki pindi wanaopoomba ajira baada ya kumaliza masomo yao kwa madai kuwa chuo hakitambuliki kwa kuwa hakina usajili.
"Kuna baadhi ya wenzetu wamemaliza chuo lakini wakienda kuomba ajira wanaambiwa chuo walichosoma hakitambuliki kwa kuwa hakijasajiliwa, hivyo tunataka kujua na sisi hatima yetu itakuaje baada ya kumaliza masomo.
"Na hata tukiuliza endapo tutamaliza masomo tutapata vyeti vya wapi maana chuo hakijasajiliwa nchini tunaambiwa vitatoka makao makuu Kampala, Uganda" alisema Jackson.
Alisema licha ya wasiwasi wa usajili, lakini uongozi wa chuo hicho umeweka ada kubwa ambayo tayari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitoa barua Novemba 13, mwaka jana kuwataka wapunguze lakini suala hilo halijafanyika hadi sasa.
Alisema matatizo mengine ni pamoja na mitaala inayotumika haijulikani kuwa ni ya nchi gani Tanzania au Uganda, kwani kumekuwa na masomo mengi pamoja na utaratibu mbaya wa utoaji wa mitihani na matokeo.
Baada ya kusikiliza malalamikio yao DC Mushi, aliwatuliza wanafunzi hao huku akiwataka wampe muda ili aweze kufutilia suala hilo kwa mamlaka zinazohusika.
"Nimesikiliza maelezo yenu na nimegundua kuwa kuna matatizo katika utendaji kwani Nacte na TCU walifanya kazi yao na hivyo Bodi ya Mafamasia wameomba niwape siku tano na mimi nawaambia mpaka Jumatatu nitakukuwa nimeshapata majibu ya kudumu ya matatizo yenu," alisema.
Septemba, mwaka jana wanafunzi hao wa KIU, walikwenda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa lengo la kumwona Waziri, Dk. Shukuru Kawambwa, lakini hawakufanikiwa kumwona.
Chanzo : MTANZANIA
Serikali yashindwa kufikia muafaka kama ilivyoahidi kufanya hivyo baada ya wiki mbili, yadai jambo hili ni gumu kutolewa uamuzi na mtu au taasisi moja,wanafunzi watinga kwa mkuu wa wilaya ya ilala 6 may 2015 kujua mustakabali wao baada ya serikali kushindwa kutoa majibu ya madai yao kwa muda walioahidi, mkuu wa wilaya adai kutokua na taarifa na kinachoendelea kampala ilihali OCD wake na mpelelezi mkuu wa kanda maalumu ya dar es salaam wanalifahamu hilo...kuna nn hapo?
pia wanafunzi wahoji hatima ya wenzao 16 waliofukuzwa mkuu wa wilaya aahidi kukutana na uongozi wa chuo na wanafunzi hao waliofukuzwa siku ya ijumaa 8 may 2015 kufahamu sababu za kufukuzwa.
Baada ya wanafunzi kumuahidi mkuu wa wilaya kwamba hawataondoka ofisini hapo hadi watakapopata majibu ya madai yao ndipo mkuu wa wilaya akalazimika kuwapigia viongozi wa taasisi husika zikiwemo NACTE,TCU,BARAZA LA WAFAMASIA na WATAALAMU WA MAABARA walionekana kurushiana mpira kati ya taasisi moja na nyingine.
Mwishowe taarifa rasmi ikawa ni kwamba kutokana na suala hili kuwa zito serikali imeshindwa kupata majibu rasmi hivyo imeamua kuunda KIKOSI KAZI kitakachofanya kazi kwa siku tano kuanzia 7 may 2015.kikosi hicho kinaundwa na wajumbe toka taasisi husika zikiwemo NACTE, TCU, HESLB, MABARAZA YA WAFAMASIA, MADAKTARI NA WATAALAMU WA MAABARA pia kitajumuisha wataalamu kutoka vyuo vingine vya afya ikiwemo MUHAS. taarifa hii ilitolewa na moja ya viongozi wa juu wa NACTE.
kwa sasa wanafunzi wameazimia kutoingia darasani kuanzia 6 may 2015 mpaka hapo madai yao ya usajili,ada na kurudishwa kwa wenzao waliofukuzwa.
Kwa wasiojua: Chancelor wa chuo hiki ni rais mstaafu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya pili DR. ALI HASSAN MWINYI.