kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Ubovu wa barabara ya Tanga-Pangani umepelekea wenye magari na madereva wao kusitisha huduma za usafiri kutoka stendi kuelekea maeneo ya Tangasisi, Bwagamoyo, Mwakidila, Mwahako, Mchukuuni mpaka Machui kuwa kwenye wakati mgumu ndani ya siku mbili.
Uchakavu wa bara bara kuanzia mabanda ya papa ni mashimo yanayopolekea kuhatarisha usalama wa wenda kwa miguu na uharibifu wa vyombo vya moto. Katikati ya barabara kuna mahandaki ya kuweza mtu kufanya makazi yake .
Ukisikiliza wananchi hasira zao za kutokulipwa fidia za nyumba zao zilizobomelewa, hasira kuu wamezielekeza kwa mbunge wa Tanga mjini na diwani wa kata ya Tangasisi kushindwa kuwajibika kutatua kero zao za muda mrefu.
Inasemekana wenye bajaji pia wanazuiwa kubeba abiria wenye, kutamba ni bodaboda kwa hizi siku mbili mishikaki kama yote!
Mjumbe hauwawi!
Tukutane 2025!