Mgomo wa madaktari na wauguzi nchini Kenya umeingia juma la pili hivi leo (siku ya Jumatatu), huku maelfu ya wagonjwa wanao tafuta huduma katika hospitali za umma wakikosa kupata matibabu.
Majimbo kumi kati ya 47 ya nchini Kenya tayari yanashiriki mgomo huo huku mengine 19 likiwemo jimbo la Nairobi palipo na jiji kuu la nchi hiyo wakitoa taarifa ya kuanza mgomo huo iwapo mazungumzo yanayo endelea yatagonga mwamba
ParsToday