Ni dhahiri kwamba wanafunzi walio wengi mijini ambako ndiko kuliko na shule/taasisi nyingi za elimu. Imekuwa ni bahati mbaya saana kwamba mgomo wa madereva umekuja kipindi kibaya sana ambapo mitihani ya sekondari kidato cha sita ikifanyika. Kwa vyovyote vile jambo hili lazima litaathiri matokeo ya mitihani inayoendelea sasa. Wengi wa wanafunzi wanatoka katika familia zilizo na maisha duni, kwamba uwezekano wa kukodi usafiri binafsi inakuwa ni tatizo. Hivyo basi, uwezekano wa wanafunzi wengi suala hili kuwaathiri kisaikolojia. Wito wangu kwa serikali ijaribu kuangalia athari zinazo patikana kwa mtu mmoja-mmoja, familia, vikundi, taasisi mbalimbali na hata Taifa kwa ujumla. Kiburi cha madaraka hakifai kabisa! Hebu shukeni chini mtatue matatizo yanayoligharimu Taifa. Leo mko hai, lakini kesho mbele ya hukumu mtajibu nini? Kumbukeni kisa cha Farao na moyo wake mgumu na majeshi yake.