Mgomo wa makuli wa bandari ya Dar es salaam 1947

Mgomo wa makuli wa bandari ya Dar es salaam 1947

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Gazeti la Uhuru la leo Jumanne 18 Desemba 2018 limachapa makala ya mwendelezo kuhusu mgomo wa makuli wa Dar es Salaam mwaka 1947 mgomo na harakati ambazo ndizo zilipelekea Abdul Sykes kuja kuunda TANU mwaka wa 1954.

1545132587555.png
 
Emu copy humu mkuu hatuoni hayo maandishi
Ili kuifanya serikali iwasikilize mahali ambapo hapakuwa na sheria za kazi, ilibidi iwekwe mikakati ambayo ingeifanya serikali iweke sheria hizo katika vitabu vyake. Kamati ndogo ya siri iliundwa na Abdulwahid akatiwa ndani ya kamati hiyo ili kuongoza mgomo uliokusudiwa. Kazi ya kamati hiyo ilikuwa kupanga na kuratibu mikakati ya kuitisha mgomo ambao ungelisaidia katika kuondoa ile dhulma iliyokuwepo. Makuli waliitisha mkutano pembeni kidogo mwa mji, mahali palipokuwa pakijulikana kama ‘’Shamba kwa Mohamed Abeid,’’ katika bonde la Msimbazi. Sehemu hii ilichaguliwa makhususi mbali na macho ya watu ili ipatikane faragha. Makuli walikula kiapo na kusoma, ‘’Ahilil Badr,’’ ili kujikinga na unafiki, usaliti pamoja na shari ya vizabizabina wangeokataa kugoma. Ubani ulifukizwa na Qur’an ilisomwa. Wakijikinga na kiapo hicho cha mashahidi wa vita vya Badr na huku wakichochewa na ushujaa wa mashahidi waliokufa katika katika vita vya Badr wakipigana na washirikina wa Makka wakiwa pamoja na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake), makuli walichagua tarehe 6 Septemba, 1947 kuwa ndiyo siku ya kuanza mgomo wao.

Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri. Watu katika mitaa jirani ya alipoishi akikaa Abdulwahid walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifanjiri moja waliposikia vishindo na makelele vimetanda mtaani. Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje. Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao. Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni. Abdulwahid, wakati ule kijana mdogo kabisa, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao. Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo. Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa.

Mgomo huo ulioenea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu. Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana. Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na Salum Abdallah Popo waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba. Chama cha African Association mjini Tabora kilimteua Mwalimu Pinda, aliyekuwa akifundisha shule ya St Mary, kuwa 'mshauri' wa wafanyakazi waliogoma. Asubuhi ya siku ya mgomo wafanyakazi wa Tanganyika Railways walikusanyika kwenye kiwanja cha mpira cha Town School, wakakaa chini ya miembe kujikinga jua. Tabora ni maarufu kwa miti hiyo. Tangu siku hiyo kiwanja hiki kikawa ndicho uwanja maalum kwa mikutano yote ya siasa.

Serikali ilimtuma kijana mmoja kutoka Masasi aliyesoma katika shule za misheni, Frederick Mchauru kuwahutubia wafanyakazi na kuwaombawasimamishe mgomo na warudi kazini. Mchauru alikuwa Mmakonde kutoka Newala. Alielimishwa St. Josephís College, Chidya na St. Andrewís College, Minaki. Mwaka 1946, Mchauru alikuwa amerudi kutoka LondonUniversity akiwa amehitimu masomo yake na kuanza kazi mjini Tabora kama Assistant Social Development Officer. Wafanyakazi waliokuwa kwenye mgomo walimpigia kelele wakimtaka anyamaze huku wakimwita msaliti. Inashangaza namna shule za misheni zilivyowatengeneza watumishi wa serikalini walio wasomi wawe watiifu na waaminifu kwa dola. Wasomi hawa mara nyingi walijikuta wanasigana na wale waliokuwa wakipinga ukoloni na udhalimu.

Mchauru alishindwa kutambua hali halisi iliyokuwapo pale sike ile. Mchauru alipuuza zile kelele akaendelea kuzungumza akijaribu kuwasihi wafanyakazi warudi kazini kwao. Ghafla hali iligeuka. Watu walipandwa na hasira na kusikia wakisema ashikishwe adabu. Watu waliokuwa wamehamaki wakaanza kumsogelea. Salum Abdallah, akiwa kiongozi wa watu wale, alihisi kuwa endapo hatachukua hatua ya kumnusuru Mchauru huenda watu wakamuadhibu. Alienda pale aliposimama Mchauru. Aliinua mikono yake juu akawataka watu watulie. Salum Abdallah alikuwa mtu wa miraba minne na alikuwa na sauti kubwa. Wanachama wengi wa TRAU wanamkumbuka kwa sauti yake, hasira zake na kwa umbo lakekubwa. Wafanyakazi walipomuona Salum Abdallah walitulia na Mchauru akaondoka pale kimya kimya kupeleka taarifa kwa hao waliomtuma kuwa watu wamegoma, hawasikii la muadhini wala la mnadi sala.
Mgomo ulienea nchi nzima na wananchi katika sekta zote kote waliweka chini zana zao za kazi. Mfumo mzima wa uchumi ulisimama. Mgomo ulidumu mwezi mzima. Wanazuoni wengi wamechambua kipindi hiki cha kuibuka kwa tabaka la wafanyakazi katika Tanganyika. Wote wamekubali kuwa ule mgomo wa mwaka 1947 ndio uliofungua ukurasa mpya katika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika. Friedland, akitathmini aina ya uongozi ulioongoza mgomo, yeye anasema:

Mgomo uliandaliwa na kamati ya siri ya makuli wasiojua kusoma; hawakujua lolote kuhusu vyama na walidhani kama wangetambulikana wangekamatwa. Baada ya kutoa madai kwa waajiri bila kufichua utambulisho wao, madai ambayo yalipuuzwa, mgomo mkubwa ulitokea.

Mgomo ule uliisababisha serikali ya kikoloni kupitisha sheria ambayo iliruhusu kuundwa na hatimae kusajiliwa kwa Dar es Salaam Dockworkersí Union. Bienefield, akifafanua mapatano yaliyofuata mara baada ya mgomo baina ya makuli na mwakilishi wa waajiri wao, anasema: Vili mwakilishi kama huyo atakavyokuja yaangalia mambo, au kutekeleza maamuzi, bila ya kuwepo chama cha wafanyakazi kinachofahamika, ilikuwa ni kitendawili

Mafanikio ya mgomo huo hayakutegemea kiwango cha elimu ya makuli, kiwango cha kujua au kutojua kusoma au kuwako kwa chama cha wafanyakazi. Mafanikio ya harakati hizo yalitegemea hasa msimamo wa Kiislam uliokuwa katika ile kamati ya siri.
 
Back
Top Bottom